img

Wanawake wakandarasi kupewa kipaumbele kanda ya ziwa ili kufikisha ndoto zao

August 5, 2021

Na Maridhia Ngemela

Serikali kuwawezesha wanawake ili kuendeleza ndoto zao hasa katika shuguli wanazofanya na kuweza kukuza uchumi utakao wasaidia.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wanawake waliohudhuria mafunzo ya wanawake makandarasi  wapatao 80 mkoani Mwanza waliotoka mikoa ya Kanda ya ziwa walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mafunzo hayo wameweza kubainisha changamoto zinazo wakabili katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Miongoni mwa washiriki waliohudhuria mafunzo hayo Christina Macha toka mkoa wa  Geita alisema kuwa mafunzo hayo yatampatia maarifa ya kiukandarasi na hivyo kumwezesha kufanya kazi hizo kwa weledi na kujiajiri na kudai kuwa mitaji ni changamoto kubwa inayowakabili katika utenfaji kazii.

Mshiki toka mkoa wa Mara Mary Kiginga alisema kuwa anashukuru serikali kwa kutoa kipaumbele kwa kundi la wanawake katika kazi hizo za ukandarasi na hivyo kuondoa dhana potofu kuwa kazi hizo ni za wanaume

 Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabra Tanzania (TANROADS) Mkoani Mwanza Mhandisi Vedastus Maribe alipokuwa akifungua mafunzo hayo alisema kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inatekeleza sera ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika ujenzi na matengenezo ya barabara hapa nchini.

Maribe amewataka wanawake hao ambao wako katika hatua za awali za ukandarasi washiriki mafunzo hayo ya matengenezo na ukarabati wa barabara kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi kwa kuwa wasikivu ili waweze kupata uelewa wa kuwawezesha kufanya kazi zao vizuri.

Wanawake hao toka mikoa ya Geita, Kagera, Mara, Simiyu na Mwanza watafundishwa namna bora ya ujazaji wa zabuni, taratibu za kusajili wa makampuni , sheria ya manunuzi, kanuni zake, namna ya kutumia mfumo wa manunuzi (TANePS) na Usimamizi wa mikataba.

“Mafunzo haya ambayo ni nadharia na kivitendo yatawawezesha kuwa tayari kusajili makampuni kwa wale ambao bado na hivyo kumudu soko la ushindani kwa kuomba kazi za ujenzi wa barabara kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa” alisema Mhandisi Maribe.

Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake Wizara ya Ujenzi Mhandisi Liberatha Alphonce alisema kuwa lengo la kushirikisha wanawake hao wakandarasi 80 katika zoezi hilo ni kuhakikisha kuwa wanaunga mkono juhudi za serikali za uendelezaji na utunzaji wa miundombinu hapa nchini.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo zaidi na kuwapa ujuzi ili wanapofanya kazi za barabara wafanye kwa weledi na kwa mujibu wa sheria zilizopo, kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa kazi za ukandarasi wa barabara.

“Mafunzo hayo ya wiki mbili yatahusu namna ya kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi ili kuwawezesha kujiajiri na kukuza vipato vyao” alisema Mhandisi Alphonce.

Alisema kuwa wanawake hao wakandarasi watapata mafunzo yao kutoka kwa wizara ya ujenzi na uchukuzi, chuo cha Teknolojia ya ujenzi (ICOT) toka mkoani Mbeya,TANROADS, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Bodi ya Usajili wa Wakandarsi (CRB).

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *