img

Olimpiki: Schoenmaker wa Afrika Kusini aweka rekodi mpya ya dunia

July 30, 2021

Kwenye Olimpiki za Tokyo, Afrika Kusini imekuwa na mshindi wake wa kwanza wa medali ya dhahabu katika kuogelea kwa kipindi cha miaka 25.

Tatjana Schoenmaker aliweka rekodi mpya ya dunia katika fainali ya wanawake ya mita mia 200.Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuogelea chini ya muda was dakika 2 na sekunde 19.

Jumanne, alishinda fedha katika mbio za mita 100.Ushindi wake wa mita 100 ulikuwa wa kwanza na muogeleaji wa kike kutoka Afrika Kusini katika kipindi cha miaka 21.

Schoenmaker alisema ana matumaini ushindi wake utaleta furaha nyumbani baada ya siku za vurugu.Afrika Kusini ilishuhudia maandamano ya vurugu kwa wiki kadhaa na uporaji wa mali uliosababisha zaidi ya watu 300 kufariki dunia na kupotea kwa mali yenye thamani ya mabilioni ya pesa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *