img

Mkuu wa USAID kutembelea Ethiopia kushinikiza kuingia kwa misaada

July 30, 2021

 

Mkuu wa shirika la misaada la Marekani (USAID) Samantha Power wiki ijayo atatembelea Ethiopia kushinikiza misaada zaidi kuruhusiwa katika eneo lililokumbwa na mizozo la Tigray, shirika hilo linasema.

Bi Power atakutana na maafisa wa serikali kutafuta suluhisho la ukosefu wa misaada ya kibinadamu kwa wale walioathiriwa na mzozo uliodumu kwa miezi tisa.Siku ya Alhamisi, mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths alianza ziara yake nchini humo kwa msukumo kama huo.Alisema kuwa mahitaji ya kibinadamu nchini Ethiopia yameongezeka kwasababu ya mzozo na mapigano ya kikabila katika maeneo mengine.

Shirika la Chakula Duniani la UN limesema kuwa wasambazaji wake wa misaada hiyo wanakaribia kuishiwa kwa kuwa malori hayangeweza kuingia katika eneo la kaskazini kwasababu ya mapigano.Aidha, kilikuwa na shambulio dhidi ya msafara wa shirika hilo mapema mwezi huu.Mamia ya maelfu ya watu huko Tigray wanaishi katika hali kama ya kukumbwa na baa la njaa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *