img

Chanjo ya Covid-19 asilimia 60 ya Watanzani

July 23, 2021

Baada ya chanjo ya Covid-19 kuwasili nchini Serikali imejiweka lengo la kuwachanja asilimia 60 ya Watanzania wote.

Waziri wa Afya, Dk Doroth Gwajima amesema awamu ya kwanza ya chanzo hiyo itatolewa kwa makundi ya mstari wa mbele ambayo yatawekwa wazi siku ya kesho.

Amesema kwa kuanzia watachanjwa watu walio kwenye mstari wa mbele lakini lengo ni kuwafikia watanzania wote watakaohitaji.

“Serikali ya awamu ya sita imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania kwa hiari yake bila malipo atapata chanjo.

“Kuhusu makundi yatakayoanza tutaweka wazi kesho ni akina nani na utaratibu upi utatumika, zitapatikana wapi haya yote tutayaeleza,” amesema Dk Gwajima

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *