img

Watu 12 wapoteza maisha kwenye mlipuko wa tanki la mafuta nchini Nigeria

April 20, 2021

Kulingana na ripoti za awali, watu 12 walipoteza maisha katika mlipuko uliotokea baada ya ajali ya kupinduka kwa tanki la mafuta kutokea katika jimbo la Benue nchini Nigeria.

Mratibu wa Jimbo la Benue wa Shirika la Kitaifa la Usalama wa Barabarani (FRSC) Yakubu Muhammed, aliliambia gazeti la eneo hilo kwamba mlipuko ulitokea baada ya tanki la mafuta kupinduka kwenye barabara ya jimbo la Oshigbudu-Obagaji.

Muhammed alisema kuwa kulingana na taarifa za awali juu ya mlipuko huo, watu 12, wakiwemo wanawake 3 na mtoto, walipoteza maisha na watu wengine wengi walijeruhiwa.

Akielezea kuwa majeruhi wengine wako katika hali mbaya, Muhammed alielezea wasiwasi wake juu ya ongezeko la idadi ya vifo.

Muhammed pia alisema kuwa nyumba na maduka ya maeneo ya jirani pia yailiharibiwa kutokana na mlipuko huo.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *