img

Walimbaka, wakaua watu wa familia yake, akawasamehe sasa wanataka tena kumuua

April 20, 2021

Dakika 39 zilizopita

Fanny Escobar

Chanzo cha picha, Daniel Pardo

Maelezo ya picha,

Mwenyewe nilikuwa nimejawa na machungu moyoni. Na leo hii saratani ndio adui wangu mkubwa. “

“Mimi ni mama wa watoto wanne lakini kwasasa nimebaki na watatu. Pia nimeasili watoto wengine wengi. Mimi ni bibi niliyejaaliwa wajukuu 9 na sasa nimepata vitukuu wawili.

Kwa miaka michache iliyopita, Fanny Escobar, kiongozi wa masuala ya jamii kaskazini magharibi mwa Colombia, hakuwa akilia.

“Sikiliza sauti yangu,” amesema. “Wakati anaulizwa anamaanisha nini, sauti yake inapotea. Mimi Silii. Silii tena.”

Badala ya kulia anapokuwa amekasirika, mikono yake huanza kutetemeka na kuingia baridi.

Baridi inamzidia Escobar wakati amemaliza mahojiano na BBC, baada ya kuelezea matukio ya kuogofya kabisa aliyopitia katika kipindi chake cha miaka 57 duniani kwenye eneo lililokumbwa na vita, Uraba.

Mateso aliyopitia ni pamoja na kubakwa, vitisho kutoka kwa wapiganaji wa vita vya msituni na wanamgambo, pia amelazimika kuhama makazi yake kutoka eneo moja hadi jingine, mauaji ya mtoto wake aliyemzaa mwenyewe, mauaji ya watoto kadhaa aliokuwa ameasili na mume wake ambaye alimnyanyasa aliporejea nyumbani akiwa mlevi.

Hata ugonjwa wa saratani aliopata umechangia mfadhaiko aliopata wakati wa vita: “Machungu yote hayo, nguo ya kujikinga niliyovaa ndio iliyoshikilia titi langu. Saratani ilikuwa imeenea. Jicho langu la kulia sasa hivi uoni wake unakaribia kufifia kabisa.

Mwenyewe nilikuwa nimejawa na machungu moyoni. Na leo hii saratani ndio adui wangu mkubwa. “

Baada ya kuulizwa anachoweza kusema kwa wale ambao pengine huenda wakahoji simulizi yake? Alijibu: “Kuna watu vijijini ambao wamebakwa mara saba, nane bado wanaendelea kubakwa kila siku katika eneo lao, (…) Simulizi yangu sio chochote ukilinganisha na kile wanachopitia maishani mwao”.

Mujeres del Planton

Chanzo cha picha, Daniel Pardo

Maelezo ya picha,

Leo hii, Escobar amekuwa tena tishio kwa wale wanaochukulia shughuli zake kama zinazoingilia mambo yao

Escobar ni kama raia wengine wa Colombia, kiongozi katika jamii yake. Anaendesha shirika lake linalopigania kusikika, pia wanapigania watoto wao wasijiingize katika uhalifu na unyanyasaji na kwa wanaojihusisha na maovu wakabiliwe na mkono wa sheria.

Leo hii, Escobar amekuwa tena tishio kwa wale wanaochukulia shughuli zake kama zinazoingilia mambo yao miongoni mwao ikiwa ni kupinga watoto wasisajiliwe katika makundi ya uhalifu.

Anatishiwa na kundi lile lile lenye kuhusishwa na wanamgambo ambalo lilikuwa chanzo cha yeye kupitia mateso aliyokumbana nayo wakati ule.

Viongozi 309 wa jamii waliuawa nchini Colombia mwaka 2020, kulingana na shirika la washauri la Indepaz. Katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka 2021, viongozi 40 wa jamii wameuawa.

Escobar anajua kuwa anatekeleza majukumu yake kama kiongozi katika nchi ya Colombia inayotambuliwa kuwa moja ya zilizo hatari zaidi duniani kutetea haki za binadamu.

“Lakini siogopi kifo,” amesema. “Huwa ninasema kila siku kwamba nilizaliwa niage dunia.”

Fanny Escobar

Chanzo cha picha, Daniel Pardo

Maelezo ya picha,

Escobar anajua kuwa anatekeleza majukumu yake kama kiongozi katika nchi ya Colombia

Miaka ya 1990, eneo hilo lilichukuliwa na wanamgambo waliosababisha vifo vya watu wengi.

” Wanamgambo hao walifanya wanachotaka lakini pia walikuwa wakatili kweli, ” amesema Escobar, na hapo akaanza kuzungumzia madhila aliyopita.

“Ghafla niliona kundi la wanaume ambalo sikujua wametoka wapi nyuma ya farasi niliyokuwa ninaendesha, wakasema kuwa dada yangu niliyekuwa naye ni mrebo sana na watarejea kumchukua,” anakumbuka.

Escobar anasema aliamua kwenda kumficha dada yake na wiki kadhaa baadaye, wanaume wale wale wakarejea nyumbani kwake alikokuwa ameolewa.

Fanny Escobar

Chanzo cha picha, Daniel Pardo

Maelezo ya picha,

Escobar anasema aliamua kwenda kumficha dada yake

Waliomba maji ya kunywa.

“Maji ya kunywa tulikuwa tunayaweka kwenye mtungi na kawaida yalikuwa baridi. Nilipoenda kuchota, wanaume wawili waliingia ndani kunifuata”.

“Nyuma ya hao, zaidi ya wanaume watano walikuwa wameingia ndani tayari. Kisha mmoja aliyekuwa amefunga kitambaa kwenye shingo yake akaanza kucheka: Akiuliza’huyu ni berraca? “.

Kwa kusema neno “berraca” – alimaanisha shupavu – wanamgambo hao wakimkejeli kwa kutaka kumlinda dada yake.

“Nikawauliza niwasaidie na nani kwasababu mzee wa boma yaani mume wangu hakuwepo?

“Wakanijibu: ‘Hapana, sisi tunakutafuta wewe.’

Walijua Escobar alikuwa peke yake. Walikuwa wamefika kumbaka.

Mujeres del Planton

Chanzo cha picha, Daniel Pardo

Maelezo ya picha,

Miaka ya 1990, eneo hilo lilichukuliwa na wanamgambo waliosababisha vifo vya watu wengi kweli.

Escobar kipindi hicho alikuwa mjamzito, na baada ya kubakwa na kundi lote hilo la wanaume, akapoteza ujauzito wake.

“Walilipiza kisasi kwa namna iliyodhuru maisha yangu… na walifaulu,” amesema.

Ubakaji ulikuwa na bado unatumiwa kama silaha ya vita.

Mateso ya Escobar hayakuishia hapo kwasababu miaka michache baadaye, wanamgambo hao hao walimuua mume wake pamoja na kijana wake, kwa kusisitiza kujua ukweli kuhusu mauaji ya baba yake.

Mwaka 2013, kundi la wanajeshi katika mji mkubwa wa Uraba, waliwabaka na kuwaua wanawake watatu barabarani.

Siku zilizofuata, kesi hiyo ilionekana kuyumba tu lakini Escobar na majirani zake waliokuwa wanawajua waliotekeleza kitendo hicho cha kinyama, waliamua kufanya maandamano makubwa kutafuta haki.

Mujeres del Planton

Chanzo cha picha, Daniel Pardo

Maelezo ya picha,

Ubakaji ulikuwa na bado ni unatumiwa kama silaha ya vita.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *