img

Umoja wa Ulaya wahofia vita kuzuka kati ya Urusi na Ukraine

April 20, 2021

 

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya amesema hatua ya Urusi kuimarisha vikosi vyake mpakani na Ukraine inaweza muda wowote kuzuwa vita kamili. 

Josep Borrel amesema Urusi ina wanajeshi zaidi ya laki moja na nusu kwenye mpaka huo. Hata hivyo, katika taarifa yake baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja huo jioni ya jana, Borrell alisema hadi sasa hakuna haja ya kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Urusi. 

Aliongeza kwamba hakuna ombi la kuzitaka nchi wanachama za Umoja wa Ulaya kujiunga na mzozo wa kidiplomasia baina ya Urusi na Jamhuri ya Czech, ambazo zimefukuziana mabalozi wao. 

Hata hivyo, mkuu huyo wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya alisema wataibebesha dhamana Urusi endapo afya na usalama wa mpinzani mkuu wa Rais Vladimir Putin, Alexei Navalny, utakuwa hatarini. 

Navalny, ambaye ana mgomo wa kula gerezani, amehamishiwa hospitalini, ambako madaktari na mawakili wake wanasema ana hali mbaya.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *