img

Ulaghai kupitia Imani: Jinsi wahubiri wenye umaarufu Nigeria,Ghana ,Afrika Kusini na DRC wanavyowahadaa waumini wao

April 20, 2021

Dakika 22 zilizopita

Wengi walishtushwa na ufunuo wa mchungaji wa Afrika Kusini aliyetumia dawa ya kuulia wadudu kuponya

Chanzo cha picha, MOUNTZION GENERAL ASSEMBLY

Uhuru wa kuabudu barani Afrika na katika maeneo mengo kote duniani umekuja na mengi mazuri .Lakini pia kuna mengine mengine ambayo yamekosa kuthibitiwa na yeyote kwa sababu kila mtu ana haki ya kuamini atakacho au kuabudu kwa njia anayoiamini .

Hata hivyo bara la Afrika katika miaka ya hivi karibuni limejipata kuwa muathiriwa wa waumini wake kutumiwa vibaya na baadhi ya wahubiri ambao wamejijengea sifa na utajiri kupitia mbinu ,vitendo na hata Imani za kustaajabisha .

Visa vya wahubiri kuwatumia vibaya waumini wao vimeendelea kukithiri na vingi hata haviangaziwi katika vyombo vya habari . Kunavyo hata hivyo baadhi ya vitendo na ‘miujiuza’ wanayodai kufanya baadhi ya wahubiri hao ambavyo vimeweza kunakiliwa na vimewashangaza watu wengi huku cha kusikitisha hata Zaidi kikiwa ukosefu wa msaada wowote kuweza kuwalinda waumini wanaojipata kama waathiriwa .

Ufichuzi kwamba Mhubiri mmoja wa Afrika Kusini alikuwa akiwapulizia usoni dawa ya kuua wadudu waumini wake kama njia ya kuwaponya uliwashtua wengi . Lakini siye pekee Afrika aliyefanya kitendo kama hicho kwa kuhusisha hatua yake hiyo na Imani ama uhuru wa kuabudu .

Miji kote barani imejaa mabango yanayotangaza makanisa, kawaida yenye majina yanayotishia mwisho wa dunia , kuahidi uponyaji wa papo hapo na wokovu kutoka kwa kila hali ama ugonjwa.

Makanisa hayo kwa kawaida huongozwa na wachungaji wenye haiba, ambao huanzisha makanisa yao badala ya kujiunga na taasisi zilizowekwa, na mara nyingi hudai kuwa na nguvu za miujiza.

Walakini, miujiza hiyo imeambatanishwa na uwezo wa waumini “kupanda mbegu” – au kutoa pesa kwa wahubiri hao . Hivi ni baadhi ya vitendo vilivyowashangaza wengi ,ambavyo vilifanywa na vinazidi kutekelezwa na baadhi ya wahubiri na manabii hao:

Sharubati ya kutibu HIV na kuwafufua watoto waliofariki

‘Nabii’ maarufu wa DRC Domique Khonde ana mamilioni ya wafuasi kote duniani na wengi wa waumini wake wanaamini kwamba sharubati yake inayouzwa kanisani inaweza kutibu kila aina ya maradhi yakiwemo virusi vya Ukimwi, Saratani na hata kuwafufua watoto waliofariki dunia .

Sharubati hiyo hutengezwa kutumia mafuta ya petrol,maji ya ndimu na viungo vingine . Khonde aliangaziwa mapema mwezi huu katika Makala ya DW yaliyozua gumzo mitandaoni kuhusu ukweli wa tiba ya ‘miujiuza’ ya sharubati hiyo ambayo chupa moja ya mililita 300 inauzwa kwa euro milioni 14 .

Mikutano yake ya kuhubiri huwavutia maelfu ya watu na katika Makala hayo imeonyeshwa jinsi watu walivyofurika uwanja mkubwa ili kumsikiliza.Inadaiwa amefaulu kutengteza mamilioni ya pesa kutokana na jusi yake hiyo na hata serikali ya DRC imemruhusu kuendelea na shughuli zake .

Miongoni mwa wafuasi wake ni viongozi wa zamani wan chi hiyo na familia zao na injili anayohubiri ni ya mafanikio .

‘ Kubadilisha Petroli kuwa sharubati ya mananasi’

Mchungaji Lesego Daniel anaongoza Rabboni Ministries katika mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria.

Aliwaamuru waumini wa kanisa lake kunywa petroli, akidai kwamba alikuwa ameibadilisha kuwa juisi ya mananasi.

Ujumbe wa tahadhari : ''Kama huwezi kubadili maji kuwa mvinyo , usijaribu haya nyumbani''

Chanzo cha picha, RABBONI CENTER MINISTRIES

Video iliyowekwa mtandaoni ilionesha muumini mmoja akimimina petroli kwenye sufuria na kisha kuiwasha ili kudhibitisha kuwa ilikuwa ikishika moto

Kisha anainywa na kusema ‘yuko sawa na hana athari zozote ‘ wakati mhubiri huyo anapomuuliza kuhusu petroli hiyo

Mwanamke anakimbizwa katika jukwaa na kupewa mafuta hayo kuyanywa kisha anasema ‘yana utamu’ hatua inayowafanya wanawake wengi kukimbilia mafuta hayo na kuyabugia .

Mhubiri wa ‘nyoka’

Penuel Mnguni wakati huo alikuwa na umiri wa miaka 25 na alikuwa akiongoza kanisa la End Times Disciples Ministries tangu mwaka wa 2014.

Awali alikuwa mfuasi wa Lesego Daniel, mhubiri wa Afrika Kusini aliyewapuzilia waumini wake dawa ya kuua wadudu .

Raia walimfukuza Penuel Mnguni katika eneo ambalo kanisa lake lilikuwepo

Chanzo cha picha, END TIMES DISCIPLES MINISTRIES

Katika mwaka aliyofungua kanisa lake picha za waumini wakila nyasi na maua kufuatia agizo lake zilisambaa katika facebook na kwenye tovuti ya kanisa hilo . Picha nyingine zilimuonyesha akiwalisha wafuasi wake mawe baada ya kudai kwamba alikuwa ameyageuza yawe mikate .

Alipewa jia ‘mhubiri wa nyoka’ baada ya kutolewa kwa picha zake akiwalisha waumini nyoka na panya akidai kwamba alikuwa amevigeuza kuwa ‘Chokolati’

Wenyeji baadaye walimfukuza kutoka mji wa Soshanguve, a kaskazini mwa Pretoria ambako kanisa lake lilikuwa

‘Kuponya upungufu wa nguvu za kiume’

Nchini Ghana Ghana, Askofu Daniel Obinim wa International Godsway Ministries ana ibada za kipekee na ghali ambazo yeye hufanya kushughulikia matatizo mbali mbali ya waumini wake .

Katika mojawapo ya kisa kinachojulikana kumhusu alionekana akiwa amesimama juu ya tumbo la mwanamke ambaye inaripotiwa alikuwa mja mzito ili kumtoa pepo kutokana na kuingiwa na pepo wachafu.

Wanaume wakitendewa miujiza

Chanzo cha picha, YOUTUBE

Katika kisa kingine alionekana akimshika mwanaume sehemu zake za siri kwa madai kwamba alikuwa akimtibu tatizo la ‘ukosefu wa nguvu za kiume’

Wanaume walisimama kwa foleni na kuinua mikoni yao ili kungoja kushikwa sehemu zao hizo kwa zamu na mhubiri huyo

Mtindo wake wa kuwaombea waumini wakati mmoja uliifanya mahakama moja mjini Accra kuripotiwa kutoa waranti ya kukamatwa kwake pamoja na washirika wake wawili baada ya kuonekana akiwaadhibu kwa viboko vijana wawili waliokuwa wamefika kanisani mwake.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *