img

Rwanda: Wakimbizi Kutoka Burundi na DR Congo wasema wenzao wanajiua kwasababu ya njaa

April 20, 2021

Dakika 4 zilizopita

The Mahama camp is home to more than 54,000 Burundian refugees

Chanzo cha picha, UNHCR

Karibu miezi miwili baada ya msaada wa chakula kupunguzwa kwa wakimbizi wanaopokea msaada katika kambi za wakimbizi walioko nchini Rwanda, sasa wanasemekana kuwa katika hatari ya kufa njaa.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana alitembelea kambi za Mahama huko mashariki, Kigeme kusini mwa nchi hiyo na na Gihembe kaskazini mwa taifa hilo , na kuzungumza na wakimbizi wa Burundi na Congo

Hapo awali, mkimbizi mmoja alikuwa na haki ya kupewa 7,600Frw kwa mwezi, kutoka Machi iliyopita mwaka huu mtu mmoja alipokea 3,040Frw, ambayo ni sawa na 100Frw kwa siku.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani , WFP / PAM, linasema kupungua huko kulitokana na “wafadhili kusitisha ufadhili wao kwa sababu ya Covid”.

Katika kambi ya Kigeme, ambayo ina wakimbizi zaidi ya 20,000, Confiance Uwamahoro, mfanyakazi wa kijamii, anasema njaa imezidi kambini kwa sababu kiasi cha Frw 3,040 ni kidogo sana na hakiwezi kuwasaidia

Uwamahoro, kutoka DR Congo, alisema: ‘Njaa imeua watu wengi. Sarafu mia moja kwa siku pia unahisi kuwa haimlishi mtu yeyote.”

Edson Munyakarambi wa kambi hiyo anasema kuna ripoti kwamba njaa imesababisha mtu mmoja kujiua na mwingine kuokolewa baada ya kujaribu kujiua kutokana kukosa chakula

“… mmoja wao alijiua na nilikuwa huko kumzika, ingawa marehemu hakusema kwanini alijiua … lakini yule mwingine ambaye alikuwa akienda kujiua alifungwa minyororo [aliokolewa] na sasa maisha yake yapo hatarini, mtu ambaye tulimuhoji alituambia alikuwa na njaa. “

Outside the Gihembe camp on a small market some are shopping

Chanzo cha picha, BBC CONNECTION

Huko Mahama wataamua kurejea

Kambi ya Mahama ni makazi ya wakimbizi zaidi ya 54,000 kutoka Burundi, pamoja na kambi ya Gihembe iliyo na zaidi ya watu 12,000 kutoka DR Congo, ambao wanasemekana kuwa katika hatari ya kufa njaa kutokana na uhaba wa misaada.

Huko Mahama, wakimbizi wa Burundi waliambia BBC kwamba idadi ya watu waliojisajili ambao walitaka kurudi iliongezeka baada ya kupunguzwa kwa msaada wa PAM.

“Niliamua kurudi nyumbani kwa sababu nilikuwa na njaa na ningekufa hapa …’ alisema Marco Minani, ambaye anajiandaa kurudi.

Emily Fredenberg, msemaji wa WFP wa Rwanda, aliambia BBC kwamba bado walikuwa wanatafuta misaada kutoka nje, na kwamba baadhi yao walikuwa wamepewa na serikali ya Canada “ambayo imefanya WFP iwe na uwezekano mdogo wa kukatiza misaada”.

“Tunatumahi kuwa katika miezi ijayo tutapata ufadhili wa kutosha kuongeza idadi ya wakimbizi, pia …”

Serikali ya Rwanda inasema kuwa kama nchi ya wakimbizi – ambao sasa ni zaidi ya 100,000 – itasaidia kuanzisha miradi ya maendeleo, kama ilivyo kwa raia wengine.

Ziara ya Filippo Grandi, Mkuu wa Ofisi ya UNHCR, inatarajiwa huko Kigali mwishoni mwa wiki hii kutoa majibu ya maswali ya wakimbizi hawa.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *