img

Rais Idris Deby wa Chad amefariki

April 20, 2021

Rais Idris Deby wa Chad amefariki wakati akiwatembelea wanajeshi walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya waasi wa kaskazini, msemaji wa jeshi amesema Jumanne siku moja baada ya Deby kutangazwa mshindi wa muhula wa sita madarakani.

Kampeni ya Deby ilisema Jumatatu kwamba alikuwa akielekea mstari wa mbele, kujiunga na vikosi vinavyopambana na magaidi. Waasi walio katika eneo la upande wa kaskazini nchini Libya, walishambulia kituo cha mpakani siku ya uchaguzi na kisha wakasonga mbele zaidi ya mamia ya kilometa upande wa kusini, kukatisha jangwa.

Deby mwenye miaka 68 aliingia madarakani katika uasi mwaka 1990 na ni mmoja wa viongozi aliyehudumu muda mrefu zaidi barani Afrika.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *