img

Morrison kuikosa Kagera kesho

April 20, 2021

Klabu ya soka ya Simba ya Dar es salaam itakosa huduma ya mshambuliaji wao Benard Morrison katika mchezo wa kesho wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Kager Sugar utakaopigwa katika uwanja wa Kaitaba.

Meneja wa kikosi cha Simba, Patrick Rweyemamu amesema Morrison ataukosa mchezo huo kutokana na kutumia kadi tatu za njano alizozikusanya katika michezo iliyopita.

Nyota mwingine wa Simba ambaye atakosekana katika mchezo huo ni Francis Kahata ambaye kibali chake kwasasa kilichopo ni kuichezea klabu hiyo katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Simba inawania alama tatu muhimu ili kuendelea kujiimarisha katika mbio za kuwania utetezi wa ubingwa ilioutwaa kwa misimu mitatu mfululizo huku ikiwa na nafasi kubwa kutokana na kuwa na mechi nyingi za viporo ambazo iwapo watashinda watawapiku vinara Yanga kwa alama saba.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *