img

Marekani yaonya hatua ya Urusi kuweka vizuizi kwenye Bahari Nyeusi

April 20, 2021

 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeionya Urusi dhidi ya kile inachosema ni “uchokozi usio sababu”, baada ya Urusi kutangaza mipango ya kuweka vizuizi kwenye sehemu ya Bahari Nyeusi, ambavyo vinaweza kuathiri njia za kuzifikia bandari za Ukraine. 

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Ned Price, inasema hatua hiyo ni ishara ya kuendelea kwa kampeni za kuihujumu Ukraine. 

Vyombo vya habari vya serikali nchini Urusi viliripoti kuwa serikali inadhamiria kuzifunga baadhi ya sehemu za bahari hiyo kwa meli za kijeshi na serikali za kigeni kwa miezi sita. 

Ikiwa hatua hiyo itatekelezwa, itazuwia kuzifikia bandari za Ukraine kwenye Bahari ya Azov, inayoungana na Bahari Nyeusi kupitia Mlango Bahari wa Kerch, mashariki mwa Rasi ya Crimea, iliyotwaliwa na Urusi mwaka 2014.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *