img

Mama wa Kiganda ambaye haoni aibu kuwa na mtoto anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja

April 20, 2021

Dakika 11 zilizopita

Person with a mask on and a rainbow sticker

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Nchini Uganda vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vinaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha maisha jela

Wakati Rita aliposikia uvumi kwamba mwanawe wa kiume anashiriki mapenzi ya jinsia moja hakuamiani.

Wakati huo, alidhani mapenzi ya jinsia moja ni laana – “tatizo” ambalo hutokea kwengine, sio nchini Uganda.

Hatimaye alipothibitisha ni kweli, alihisi kana kwamba kitu kibaya kimevamia boma lake.

“Nilipothibitisha, Nililia. Nililia kwasababu sikuamini… Nilijifungia ndani na kulia sana,” aliambia BBC.

Ukatili wa Uganda dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ni jambo linalojulika.

Kushiriki mapenzi ya jinsia moja ni kosa ambalo hukumu yake ni kifungo cha Marsha gerezani, na watu walio katika uhusiano wa aina hiyo wanabaguliwa, kutishiwa na kunyanyaswa katika jamii.

Lakini juhudi za kupigania haki ya wapenzi wa jinsia moja ni hali ambayo inachukuliwa kuwa na pande mbili hasimu zilizo na misimamo mikali – Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na jamii inayopinga mapenzi hayo.

Uhalisia wa hali hii unajitokeza vibaya, wakati wazazi kama Rita wanapojipata katikati ya mzozo – kati ya imani waliyokuwa nayo na hali ya wapendwa wao.

‘Uvumi kumhusu mwanangu wa kiume’

Kundi moja nchini Uganda linajaribu kuwasaidia wazazi kama Rita kuelewa na kuwakubali watoto wao, na kukabiliana na changamoto za kuishi na ushoga.

Rita alipata uvumi kuhusu hali ya mwanawe wa kiume kutoka kwa rafiki, ambaye alisikia watu wakisema anashiriki mapenzi ya jinsia moja.

Alipata usumbufu wa akili na kwanza kufikiria kama kulikuw ana dalili lakini hakuziona.

Hatimaye mwanawe alimthibitishia kwamba ni kweli anashiriki mapenzi ya jinsia moja.

Marafiki na majirani walipoendelea kuzungumzia familia yake, Rita alijifungia ndani kuepuka fedheha, huku mume wake akimlaumu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kama mama.

Baada ya kuwaza na kuwazua, anasema “alijiliwaza”, alipogundua hakuna mtu mwingine atakaye simama na mwanawe wa kiume, na halo akaanza kutafuta njia za kukabiliana na hali hiyo.

Wakati mwingine Rita alijipata peke yake alipohitajji ushauri a usaidizi. Mambo yalibadilika wakati mwanawe wa kiume aliposikia kuna kundi linalowasaidia watu kama yeye, na kumsihi ajiunge nao.

Kundi hilo linafahamika kama PFLAG Uganda, ambalo linamaanisha Simama na Wazazi na Familia ya Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Lengo la kindi hilo ni kutengeza mazingira salama ambapo wazazi wanaokabiliwa na changamoto hizo wanaweza kuja pamoja, kuuliza maswali na kuzungumzia masuala ambayo hawangedhubutu kujadili katika hali ya kawaida.

Mwanzilishi wa kindi hilo Clare Byarugaba, amejitangaza hadharani kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja na ni mwanaharakati ambaye ameamua kutetea haki ya wapenzi wa aina hiyo kutokana na hali aliyokumbana nayo katika familia yake binafsi.

Clare aliangaziwa na jarida moja nchini humo kabla afahamishe familia yake kuhusu hali yake. Hakutoa angalizo, na hakuwa na namna ya kuwaandaa wazazi kujua ukweli na jinsi ya kukabiliana na aibu iliyotokana na ufichuzi huo kuhusu maisha yake.

Ugandan swimmer Clare Byarugaba poses during the swimming competition at the 2018 Gay Games

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Clare Byarugaba alishiriki michezo ya wapenzi wa jinsia moja ya Paris mwaka 2018 miaka minne baada ya kuandikwa vibaya na gazeti

Moja ya changamoto kudu inayowakabili wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda, ni kutengwa kwa familia zao.

Clare anasema mahali salama kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja katika nchi ambayo jamii inapinga vikali mahusiano ya aina hiyo ni nyumbani kwao, ambapo wanaweza kujisikia huru na kukubaliwa kabisa.

Lakini kufikia hilo, Clare aligundua kwamba wazazi wanahitaji kupewa usaidizi pia.

Aliwasikitikia wazazi wake katakana na changamoto walizopitia kwa kuwa,wazazi wa binti msagaji – hali inayochukuliwa kuwa chanzo cha aibu kubwa nchini Uganda.

Sio mmoja tu

Aligundua kuwa aina ya msaada na mshikamano alioweza kutumia ndani ya jamii ya LGBTI haikupatikana kwa wazazi, ambao uzoefu na mitazamo yao ilikuwa tofauti sana.

Clare aliangalia harakati za PFLAG ambazo zilianzia Marekani, na kuibadilisha ili iendane na muktadha wa eneo hilo.

Lengo lilikuwa kubuni mazingira salama itakayowaleta pamoja wazazi kuzungumza na wataalamu wa mauala ya kisaikolojia na viongozi wa kidini walio na misimamo ya kadri, pamoja na wadi wenzao.

Mikutano inaendeshwa kwa kugha ya Kiganda, huku kundi hilo likitoa maelezo sahihi kuhusu mapenzi ya jinsia moja na ushauri wa namna ya kukabiliana na changamoto katika mazingira yanayopinga vikali uhusiano wa aaina hiyo.

Kundi hilo lilikutana mara ya kwanza mwisho wa mwakaf2019, ambapo akina mama wanna na baba mimosa walihudhuria kikao.

Kila mwanachama alisimulia kisa chake – jinsi alivyogundua mwanawe anashiriki mapenzi ya jinsia moja, jinsi alivyopokea taarifa hizo na masiva yanavyoendela baada ya kugundua hilo.

line
line

Clare anakumbuka kuona wazazi walivyoingia chumba cha mkutano wakiwa wanyonge. Na jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza, lakini wakabaini visa vyao vinafanana na kujihisi hawakuwa peke yao.

Alielezea hisia zao katika mkutano huo sawa wazazi waliokuja pamoja kuomboleza watoto wao.

Rita alikuwa mmoja wa wanachama wa kwanza wa kikundi hicho na kuhudhuria mikutano hiyo kulibadili mtazamo wake:

Si kuamini shirika hilo linatujali hata sisi wazazi.

“Nilifurahi sana kuwaona wazazi wengine kama mimi wakikaa meza moja. Kila unayemwangalia amezaa mtoto kama wangu.”

1px transparent line

Msaada wa wazazi wengine umenisaidia kuacha kusikiza maneno ya watu na kuimarisha tena uhusiano wa mama na mwanawe ambao alihisi ulikuwa umesambaratika.

Pia alianza kumpatia ushauri kuhusu uhusiano,sawa na watoto wake wengine.

Clare anasema matokeo ya juhudi za kundi hilo zinajitokeza katika mabadiliko madogo kama vile lugha ya heshima inayotumiwa na wazazi.

“Mwanzoni walikuwa wanatumia maneno ya kudhalilisha wanapowazungumzia watoto wao.” Sasa lugha yao imebadilika: “Naam huyo ni mwanangu, Naam huyo ni mwanangu.” alisema.

Kwa wanachama wengine kama Rita,kuwaekewa watoto wao binafsi kumewafanya wazazi wengine kuwa na mtazamo tofauti kuhusu jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda.

Ikizingatiwa kwamba mwanzoni alidhani kuwa mahusiano ya aina hiyo ni laana, Rita saga anawajali na kuwatunza watu hao.

*Jina la Rita limebadilishwa kulinda utambulisho wake

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *