img

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko na maporomoko

April 20, 2021

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko na maporomoko yaliyosababishwa na mvua kubwa imeongezeka hadi 181  nchini Indonesia.

yaliyosababishwa na mvua kubwa imeongezeka hadi 181  nchini Indonesia.

Naibu Gavana wa jimbo la Mashariki la Nusa Tenggara, Josef Nae Soi, amesema kuwa juhudi za hivi karibuni za utaftaji na uokoaji zimepelekea kupatikana kwa miili zaidi.

Akibainisha kuwa jumla ya vifo vimeongezeka hadi 181, Josef amesema kuwa utaftaji wa watu 48 unaendelea.

Mvua, ambazo zilianza kunyesha tangu Aprili 5 katika miji ya East Flores, Lembaga na Alor katika jimbo la Mashariki ya Nusa Tenggara, zilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Baada ya mafuriko na maporomoko ya ardhi, karibu nyumba elfu 15 zimeangamia.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi mara nyingi hutokea Indonesia katika ukanda wa ikweta, haswa kati ya Oktoba na Aprili.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *