img

Watu 11 wafariki katika ajali ya treni Misri

April 19, 2021

Maafisa nchini Misri wanasema ajali ya treni ya abiria kaskazini mwa Cairo imeua watu wasiopungua 11. Mamlaka ya reli inasema kwamba mabehewa manne ya gari moshi yalitoka nje ya reli katika jiji la Banha katika mkoa wa Qalyubia Jumapili.

Wizara ya Afya inasema katika taarifa kwamba walau watu wengine 98 walijeruhiwa. Video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha mabehewa yakipinduka na abiria wakikimbilia usalama kando ya reli.

Treni hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda mji wa Nile Delta wa Mansoura kutoka mji mkuu wa Misri. Ilikuwa ni ajali mpya ya reli kuikumba nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *