img

Vyama vya kihafidhina vyashindwa kuamua mrithi wa Merkel

April 19, 2021

 

Vyama vya kihafidhina hapa nchini Ujerumani vimeshindwa kufikia makubaliano ya mtu atakayechukuwa nafasi ya Kansela Angela Merkel, baada ya muda wa mwisho vilivyojiwekea kumalizika usiku wa kuamkia leo. 

Chama cha Kansela Merkel cha CDU na mshirika wake CSU cha Bavaria vimekuwa kwenye mvutano mkali wa kuamuwa mgombea wao wa kiti cha ukansela kwenye uchaguzi wa baadaye mwaka huu.

Wajumbe wenye nguvu kwenye vyama hivyo walikuwa wanawashinikiza wagombea wawili wakuu kumaliza tafauti zao, wakikhofia kwamba mpasuko baina yao unaweza kuhujumu uwezekano wa kurejea madarakani kwa muhula wa tano mfululizo katika uchaguzi wa Septemba. 

Armin Laschet, kiongozi wa sasa wa CDU na waziri mkuu wa jimbo lenye watu wengi la Northrhine Westphalia, na Markus Soeder, mkuu wa CSU na pia waziri mkuu wa jimbo lenye utajiri la Bavaria, ndio vinara wa mkwamo huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *