img

Vitendo vinavyofanywa vikiendelea Tasnia ya muziki tunaipoteza – Majizzo

April 19, 2021

 Mkurugenzi wa E-FM na TV-E, Majizzo amepaza sauti yake kukemea kwa uchungu yanayoendelea kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva, Majizzo amefunguka hayo leo kupitia mahojiano na kipindi cha Joto Kali La Asubuhi ndani ya E-FM na TV-E.

“Mienendo au vitendo ambavyo vinafanywa kwenye muziki vikiendelea, tasnia tunaipoteza. Hii naomba niongee kwa uchungu sana, wapo watu wengi walijitoa kwenye hii tasnia ya muziki na haikuwa rahisi. Mwanzoni kabisa, wazazi wetu au Kaka zetu walikuwa hawataki vijana wengi tujihusishe na muziki, Mimi mmoja wapo nilipata shida kuishawishi familia yangu.

“Juhudi za Master J, sasa hivi akiona vitu kama hivi anaumia kiasi gani mtu ambaye alikuwa anakesha 24/7 kuwa andaa wanamuziki, na ilikuwa hailipi zaidi ya kutengeneza heshima. Leo anaona nguvu zangu na akili zangu zote ambazo nilikuwa naziweka pale, haya ndio matunda.” alifunguka Majizzo na kuwataja Watayarishaji kama Enrico wa Sound Crafters na Majani

Aliendelea zaidi kwa kusema; “Tumepambana, tumepigana kwenye njia zote za maumivu, Jasho, akili hadi kufikia hatua sasa hivi muziki ni biashara ambayo wao inawatengenezea hela, baada ya kuifanya biashara tunataka kurudi kule nyuma kuwaaminisha wazee kwamba walikuwa sahihi, Muziki ni Uhuni.

“Imefika point muziki hauwezi kwenda bila kufanya Matukio ya kawaida. Unamkumbuka Daz baba na wimbo wa ‘Umbo Namba 8’ alifanya kitu gani cha kujizalilisha ili wimbo uwe mkubwa? Picco wa ‘Kikongwe’ Ferooz ‘Starehe’ Nachotaka kusema tuache kufanya vitu vingine vya ajabu kwa sababu ya Ku-support muziki, tufanye Muziki mzuri.”

“Huwa naongea sana Mhe. Waziri, namwambia tusisubiri mpaka hali iwe mbaya na tuchukue hatua. Tuchukue hatua sasa hivi ili kuokoa Kizazi kinachokuja. Ikiwezekana tutofautishe kati ya BASATA na Serikali, wakati mwingine tunawabebesha BASATA mzigo ambao sio wa kwao. Unakuta ni ishu ya Criminal ‘JINAI’ tunaiangalia BASATA, Jinai ni Jinai, BASATA hawana Cha kufanya na Jambo la Criminal” – Majizzo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *