img

TAKUKURU Manyara yapokea malalamiko 189 ya Rushwa

April 19, 2021

 

Na John Walter-Manyara.

Tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara imesema Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka 2021, ilipokea jumla ya malalamiko 189 ambapo kati ya malalamiko hayo, 122 yalihusiana na makosa ya rushwa na  67 yalihusu makosa mengine ambapo walalamikaji walishauriwa na kuelekezwa katika ofisi husika kwa ajili ya utatuzi wa malalamiko yao.

Mkuu wa Takukuru mkoani hapa Holle Makungu amesema jumla ya kesi mpya zilizofikishwa Mahakamani ni tano.

Makungu amewataka Watanzania wote kwa ujumla kuwa ibara ya 13 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,imetoa usawa mbele ya sharia.

Aidha amezikumbusha mamlaka zote za nchi  kuwahudumia watu wote kwa msingi huo bila kujali utaifa wao,kabila, mahali walipotokea, maoni yao kisiasa rangi dini jinsia au hali yao ya maisha.

Amerejea ibara ya 107A na 107B za katiba hiyo ambapo zimetoa mamlaka kwa mhimili wa Mahakama kuwa na kauli ya mwisho ya utoaji haki katika nchi ya Tanzania ambapo kwa mujibu wa ibara hizo uhuru wa Mahakama katika kutoa haki ya kila mmoja umefafanuliwa.

Pia Takukuru Manyara kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2021, kesi nne zilitolewa hukumu ambapo kati ya hizo kesi tatu washtakiwa walipatikana na hatia na kupewa adhabu kwa mujibu wa sharia na kesi moja mtuhumiwa aliachiliwa huru na kesi 39 zinaendelea mahakamani zikiwa katika hatua mbalimbali.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *