img

TAKUKURU Manyara yaokoa Mamilioni ya fedha na Mali

April 19, 2021

Na John Walter-Manyara.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Manyara imefanikiwa kuokoa shilingi Milioni 32,400,434.00 pamoja na mali mbalimbali ambazo ni Magari manne,Trekta moja,Pikipiki moja pamoja  jembe la kukokotwa na Ng’ombe katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka Januari hadi Machi 2021.

Mkuu wa Takukuru mkoani hapa Holle Makungu amesema hilo limewezekan baada ya kufanya operesheni za kiuchunguzi zilizolenga kurejesha fedha za Serikali zilizokuwa zichepushwe au kufanyiwa ubadhirifu kinyume na sharia ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mkungu ameeleza kuwa kati ya fedha zilizookolewa kiasi cha shilingi milioni 14,571,200.00 ni fedha za vyama vya ushirika yaani Saccos na Amcos, Milioni 10,504,000.00 zilirejeshwa kwa wanyonge ambao walikuwa wamedhulumiwa haki zao na milioni 7,325,234.00 zilirejeshwa serikalini.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *