img

Mawaziri wa EU wasema Navalny sharti apate matibabu

April 19, 2021

 

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell amesema umoja huo unaitwika dhima serikali ya Urusi kuhusiana na hali ya afya ya mkosoaji mkubwa wa serikali hiyo Alexei Navalny. 

Borell amesema hayo mnamo wakati mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya, wanatarajiwa kukutana leo kwa njia ya video kwa mazungumzo kuhusu afya ya Alexei Navalny ambayo inatajwa kuwa mbaya. 

Zaidi kuhusu hilo Borell amesema “Tuna wasiwasi mwingi kuhusu afya ya Navalny. Jana tulitoa taarifa kwa niaba ya nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya tukiitaka serikali ya Urusi kumpa huduma za matibabu anazohitaji. 

Wanawajibika kwa usalama wake.” Wafuasi wa Navalny wameitisha maandamano makubwa nchini kote siku ya Jumatano, yanayotarajiwa kufanyika saa chache tu kabla ya hotuba ya Rais Vladimir Putin kuhusu hali ya nchi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *