img

Marekani: Urusi itapata ‘athari’ iwapo mkosoaji mkubwa wa Rais Putin, Alexei Navalny atafariki gerezani

April 19, 2021

Marekani imeonya Urusi kwamba itakabiliwa na “athari” mwanaharakati wa upinzani Alexei Navalny akifariki jela.

Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Muungano wa Ulaya pia wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya Bw. Navalny.

Madaktari wake wanasema Navalny “atafariki siku chache zijazo” ikiwa hatapewa matibabu ya dharura ya kuumwa na mgongo na mguu kufa ganzi.

Balozi wa Urusi nchini Uingereza amesema Navalny anatafuta sifa na “hataruhusiwa kufa jela”.

Navalny ambaye ni mkosoaji mkuu Rais Vladimir Putin, alifungwa jela mwezi Februari kwa makosa ya zamani ya ubadhirifu, ambayo anadai yamechochewa kisiasa.

Alianza mgomo kula tarehe 31 mwezi Machi kulalamikia hatua ya kuzuiliwa kupata tiba, hivi karibuni madaktari wake walisema vipimo vya damu alivyofanyiwa hivi karibuni vinaashiria figo zake huenda zikaacha kufanya kazi, hali ambayo inaweza kumfanya akapatwa na mshtuko wa moyo wakati wowote.

Siku ya Jumapili , nchi kadhaa zilijiunga na Jumuia ya kimataifa kupinga matendo maovu dhidi ya Navalny ndani ya jela ya Urusi katika mji wa Pokrov, karibu kilo mita 100 (sawa na maili 62) mashariki ya Moscow.

Mshauri Marekani wa usalama wa kitaifa wa usalama Jake Sullivan ameiambia CNN kwamba kutakuwa na “athari ikiwa Bw. Navalny atafariki” na Urusi “itawajibishwa na jumuia ya kimataifa”, huku Rais Joe Biden akisema hatua ya kumzuia kupata huduma za matibabu “inasikitisha na haifai kabisa”.

Marekani tayari imekuwa ikizozana kidplomasia na Urusi kufuatia shambulio la sumu ya neva aina ya Novichock dhidi ya Navalny mwaka uliopita.

Kremlin amepinga madai ya Navalny kwamba Rais Vladimir Putin aliagiza shambulio hilo. Lakini maafisa wa intelijensia wa Marekani walijiridhisha kuwa serikali ya Moscow ilihusika na tukio hilo, kuufanya utawala wa Biden kuwawekea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Urusi.

Viongozi wa EU wanatarajiwa kujadili suala hilo leo Jumatatu, na Josep Borrell, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa muungano huo, amesema EU ina “wasiwasi mkubwa” na kutoa wito kwa mamlaka ya magereza kutoa idhini ya Navalny kupata huduma ya matibabu mara moja.

Katika taarifa afisi ya Uingereza ya masuala ya kigeni imesema: “Bwana Navalny lazima apewe huduma huru ya matibabu. Tunataka achiliwe huru kutoka gerezani ambako anazuiliwa kwa maslahi ya kisiasa.”

Binti wa Navalny, Daria Navalnaya,20, ambaye ni yuko masomoni California, aliandika “mpatieni idhini daktari amhudumie baba yangu ” kwenye Twitter.

Mke wa Navalny, Yulia alisema amepoteza kilo tisa tangu alipoanza mgomo wa kula chakula, kwa mujibu wa shirika la habari la AP.

Wafuasi wa Navalny nchini Urusi wanaandaa maandamano ya kitaifa Jumatano wiki hii kuwasilisha ujumbe kwamba “kuna hali ya dharura ambayo inahitaji kushughulikiwa haraka iwezekanavyo, la sivyo kitu kibaya kitatokea”.

Viongozi wa EU wanatarajiwa kujadili suala hilo leo Jumatatu, na Josep Borrell, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa muungano huo, amesema EU ina “wasiwasi mkubwa” na kutoa wito kwa mamlaka ya magereza kutoa idhini ya Navalny kupata huduma ya matibabu mara moja.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *