img

Malawi : Rais Chakwera awafukuza kazi waziri na maafisa waandamizi

April 19, 2021

Rais amesema hatua yake inafuatia ukaguzi aliyoamrisha ufanywe kuhusiana na matumizi ya karibu dola milioni 7.8 kwa ajili ya shughuli za janga la Corona.

Alisema hakutakuwa na mtu atakae samehewa akisisitiza kwamba zaidi ya maafisa darzeni moja wamehusika kutokana na ripoti ya mkaguzi.

Miongoni mwao wakiwemo maafisa katika ofisi ya Rais na Baraza la Mawazirti ambao tayari wameshakamatwa.

Rais aliahidi kutakuwa na watu zaidi watakao kamatwa miongoni mwa wafanyakazi wa serikali.

Waziri wa kazi ametuhumiwa kutumia fedha za kushughulikia COVID-19 kwa ajili ya kulipia matumizi ya safari zake Afrika Kusini.

Rais Chakwera anasema ingawa waziri alirudisha hizo fedha lakini inamaana kwamba zilipohitajika hazikuwepo.

Wakati huo huo polisi wa Malawi wamethibitishwa kukamatwa kwa watu 19 wanaotuhumiwa kutumia vibaya fedha za COVID-19.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *