img

Luis Miquissone anyakua Tuzo ya mchezaji bora

April 19, 2021

 

Mchezaji wa Simba, Luis Miquissone ameteuliwa kuwa mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara kwa mwezi Machi.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Bara, TPLB imemtambulisha nyota huyo kuwa mchezaji bora ndani ya Machi.

Kiungo huyo amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Anakumbukwa kwa kupachika bao la dakika za lala salama mbele ya Tanzania Prisons ambalo liliwapa pointi moja mabingwa hao watetezi kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Amewashinda Idd Seleman, ‘Nado’ wa Azam FC na Paul Nonga wa Gwambina FC.

Luis kwa mwezi Machi aliweza kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *