img

Ligi mpya ‘Super League’ yaibua mvutano

April 19, 2021

 

Chama cha Vilabu vya Soka Barani Ulaya, ECA, kimesema kinapingana vikali na mipango ya viongozi wa klabu 12 kubwa kabisa barani humu kuanzisha ligi yao waliyoipa jina la Super League. 

Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo na ECA inasema chombo hicho kinachowakilisha timu 246 barani Ulaya kinaendelea kuheshimu muundo wa mashindano kama uliyoamuliwa na Shirikisho la Soka la Ulaya, UEFA. 

Timu 12 kutoka England, Uhispania na Italia zilitangaza hapo jana kwamba zinakusudia kuwa na ligi ya peke yao, uamuzi ambao umekosolewa pia na UEFA, Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, pamoja na mashirikisho ya soka kwenye mataifa hayo matatu. 

Miongoni mwa klabu hizo zinazounda ligi hiyo mpya ni Juventus, ambayo mkuu wake Mtaliano Andrea Agnelli, ndiye pia rais wa ECA. Hata hivyo, klabu ya Juventus imethibitisha kujitoa kwenye chama cha ECA na kiongozi wake Agnelli amejiuzulu rasmi wadhifa wake wa urais wa chama hicho.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *