img

Flick Atangaza Kuondoka Bayern

April 19, 2021

 

KOCHA wa Bayern Munich, Hansi Flick ameiambia klabu yake kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Flick ambaye mkataba wake unamalizika Juni 2023, alisema hayo baada ya kikosi chake kuifunga Wolfsburg 3-2 na kuwa pointi saba kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Awali, akiwa kocha msaidizi, Flick, 56, aliichukua timu hiyo Novemba mwaka 2019 na kushinda taji la Bundesliga na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika msimu wa kwanza wa kuifundisha timu hiyo.

Kocha huyo amekuwa katika mapambano ya madaraka na mkurugenzi wa soka, Hasan Salihamidzic.

Flick pia amekuwa akihusishwa sana na timu ya taifa ya Ujerumai wakati Joachim Low akijiandaa kuondoka baada ya mashindano ya sasa ya mataifa ya Ulaya.

Bayern pia ilitwaa taji la klabu la Dunia Februari, huku likiwa taji lake la sita kwa Flick katika miezi 16 ya kuifundisha timu hiyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *