img

Chama tawala cha Cuba chabadili uongozi

April 19, 2021

Wajumbe wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba wameichaguwa Kamati Kuu mpya, hatua muhimu kabisa kwenye mageuzi ya utawala wa taifa hilo la Amerika Kusini. 

Ujumbe wa Twitter wa chama hicho unasema wajumbe wa Kamati Kuu watachaguwa uongozi wa chama utakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitano baina ya sasa na 2026.

 Kuondoka kwake kama katibu mkuu wa chama, nafasi yenye nguvu kabisa nchini Cuba, kunahitimisha miongo sita ya familia ya Castro kwenye utawala iliyoanzia kwa mapinduzi yaliyoongozwa na kaka yake, Fidel, aliyekufa mwaka 2016. 

Wakati kizazi cha baada ya mapinduzi kikichukuwa madaraka. Castro atakabidhi wadhifa wake kwa Rais Miguel Diaz-Canel, mwenye umri wa miaka 60. 

Viongozi wengine muhimu wanaostaafu ni Jose Ramon Machado Ventura, mwenye umri wa miaka 90 na anayechukuliwa kama mtu wa pili kwa umuhimu nchini Cuba; na Kamanda Ramiro Valdes, mwenye umri wa miaka 88.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *