img

Chama cha watetezi wa mazingira chapata mgombea wa Ukansela

April 19, 2021

 

Chama cha Kijani nchini Ujerumani, kimemtangaza muasisi mwenza wa chama hicho Annalena Baerbock kuwa mgombea wake wa kwanza wa kiti cha ukansela wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao mwezi Septemba mwaka huu.

Muasisi mwengine Robert Habeck ametangaza kuteuliwa kwa Baerbock mwenye umri wa miaka 40 leo Jumatatu. Uteuzi wa Baerbock sasa unasubiri kuidhinishwa na kamati kuu ya chama hicho mnamo mwezi Juni.

Mchakato wa chama hicho cha watunza mazingira umefanywa kwa njia tulivu bila mvutano, tofauti na jinsi ambavyo hali imekuwa katika chama cha wahafidhina cha CDU chake Kansela Angela Merkel na chama mshirika kutoka Bavaria CSU, ambavyo muda walivyojiwekea umemalizika huku vikiwa vimeshindwa kufikia makubaliano.

Wajumbe wenye nguvu kwenye vyama hivyo walikuwa wanawashinikiza wagombea wawili wakuu kumaliza tafauti zao, wakihofia mpasuko baina yao unaweza kuhujumu uwezekano wa kurejea madarakani kwa muhula wa tano mfululizo katika uchaguzi wa Septemba. 

Armin Laschet, kiongozi wa sasa wa CDU na waziri mkuu wa jimbo lenye watu wengi la Northrhine Westphalia, na Markus Soeder, mkuu wa CSU na pia waziri mkuu wa jimbo lenye utajiri la Bavaria, ndio vinara wa mkwamo huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *