img

Afya ya uzazi: ‘Siwezi kumuambia mama yangu kuwa ninafanya mapenzi’

April 19, 2021

Dakika 16 zilizopita

A silhouette of a couple

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Huduma zinazotolewa za afya ya ngono kuanzia mwaka jana nchini Singapore

Wakati mkaazi wa Singapore Nadia ambaye sio jina lake halisi, alipotembelea kliniki kupimwa kama amepata maambukizi ya ugonjwa wa zinaa miaka mitatu iliyopita, aliondoka kwa daktari akiwa na aibu kweli.

Anasema daktari aliyekutana naye, mwanamke mtu mzima alimuongelesha vibaya na kumrushia vijipeperushi “kana kwamba mimi ni mjinga”, anakumbuka mwanafunzi huyo mwenye miaka 24.

“Nilihisi mtu amenihukumu vibaya mno – kana kwamba lilikuwa kosa langu kupata maambukizi kwasababu sikustahili kufanya mapenzi,” amesema.

Lakini sasa hivi, kuna huduma zinazotolewa za afya ya ngono kuanzia mwaka jana nchini humo kupitia mtandaoni.

Wanaruhusu watu “bila aibu yoyote” kufikia huduma za afya ya ngono na pia kupata ushauri – jambo ambalo vijana wadogo kama vile Nadia wanasema wanazihitaji hasa ikizingatiwa kuwa mtazamo wao juu ya suala la hilo ni tofauti kabisa ikilinganishwa na mtazamo wa watu wa kizazi kilichopita.tambo.

Na sasa Nadia anasema yeye anatumia huduma za kampuni moja inayotoa huduma hizo ikiwemo kupima magonjwa ya zinaa kwa njia ya faragha.

Kampuni hiyo inachofanya ni kuagiza wateja wake kuchukua vipimo fulani na kuvituma ili ivifanyie uchunguzi na mteja anarejeshewa majibu yake baada ya siku mbili au tatu.

Ni kawaida kwa vijana kuishi na wazazi wao kabla ya kuolewa au kuoa kwa sababu ya utamaduni ambao umekuwepo na wengine kutokana na misingi ya kidini.

“Familia yangu ni ya kitamaduni – ni raia wa Singapore na pia ni Muislamu wa Malay, kwa hivyo kuna mambo fulani yanayotarajiwa kutoka kwako. Siwezi kumuambia mama yangu kuwa ninashiriki ngono,” Nadia amesema.

Ingawa njia wanayotumia kutoa huduma huenda ikawa sio ya uhakika, ndio pekee ambayo vijana wengi wa Singapore wanaiona kama mkombozi wao kupata huduma hizo na taarifa za afya ya ngono.

Women holding birth control pills

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kumuuliza mhudumu wa afya katika eneo lako kuhusu mbinu za kupanga uzazi ni “aibu” au “kibarua kigumu”

‘Nilihisi kudhalilishwa’

Wayne*, 37, ametumia kampuni moja inayotoa huduma za afya ya ngono kwa wanaume mtandaoni, kukabiliana na tatizo lake la kumaliza mapema wakati anafanya tendo la ndoa.

“Tatizo hili ni kama kunywa dawa wakati unaumwa na kichwa. Lakini wanaume wengi wanaogopa kwenda kwa daktari na hata kukubali kwamba wana tatizo hilo.

Lakini baada ya kwenda kumuona daktari miaka miwili iliyopita, kulimfanya hata kujihisi vibaya hata zaidi.

“Baada ya kwenda hospitali, daktari na muuguzi wake walikuwa wananiuliza maswali kwa sauti ya juu tena mbele za watu nina tatizo gani. Nilihisi kudhalilishwa kweli.”

Anasema akilinganisha huduma aliyopokea mara ya kwanza na ile aliyopata katika huduma ya mtandaoni anahisi ya mtandaoni imetolewa kwa njia ya “heshima” kwake yeye kama mgonjwa.

“Huduma zilikuwa nzuri ikilinganishwa na zile za kukutana na daktari moja kwa moja kwasababu dunia nzima haikujua kile ninachopita.”

Demand for sex toys is increasing in China, the world's biggest exporter of bedroom aids, partly thanks to the coronavirus

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Huduma za afya ya ngono kwa vijana zinaendelea kupata umaarufu mkubwa.

Changamoto za kupata huduma za afya ya uzazi kwa vijana

Vijana kujizuia kufanya ngono bado imekuwa changamoto kubwa hata baada ya baadhi ya nchi kutoa elimu ya ngono kwa wanafunzi.

Na hivyobasi imekuwa vigumu kwa vijana kwenda kutafuta huduma hizo moja kwa moja kwa daktari kwasababu ya vile wanavyohudumiwa na kuachwa wakijihisi kuwa na aibu na kutowajibika.

Kwa upande mwingine, pia imekuwa changamoto zaidi kwa wazazi kujitokeza hadharani na kuzungumzia suala hilo na vijana wao.

Huduma za afya ya uzazi kwa vijana katika nchi hizo zinaendelea kupata umaarufu mkubwa.

Vijana wanajali sana kuhusu afya yao ya uzazi na wanaendelea kutafuta njia za kuwajibika licha ya vikwazo vinavyowakabili, kulingana na kituo kimoja cha eneo kinachotoa ushauri kwa vijana.

“Hawataki kuuliza maswali kuhusu ngono, isipokuwa tu pale wanapohisi wako salama kuzungumzia suala hilo. Na huduma za kidigitali za afya ya ngono kwa vijana huenda ikawa jukwaa muafaka katika kukabiliana na changamoto hii.”

Nadia anakubali kwa kusema kuwa licha ya mila na desturi zilizopo, alijua kuna umuhimu wa kwenda kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara, hasa wakati ambapo alikuwa anataka kuanza mahusiano mapya.

“Hii ndio njia pekee ya kuonesha uwajibikaji, lakini najua kuna wengi ambao hawawezi kupata huduma hizi kwasababu naelewa hali ilivyo, haijakuwa rahisi.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *