img

Utekelezaji wa amri ya kutotoka nje ya Nairobi – maelfu walikwama kwenye barabara za jiji

April 18, 2021

Dakika 4 zilizopita

Msongamano wa magari

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelfu ya waendesha magari na wasafiri walijipata mashakani usiku wa Jumamosi baada maafisa wa usalama jijini Nairobi kufanya oparesheni ya kuhakikisha wakazi wa jiji wanazingatia sheria ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi afajiri.

Hakuna magari yaliyoruhusiwa kuingia au kutoka katika mji mkuu.

Katika baadhi ya barabara polisi waliwaagiza waendesha magari kuzima injini, kutoka ndani ya gari na kukaa kandao ya barabara.

Kanda za video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zilionesha msongamano mkubwa wa magari huku baadhi ya magari yanayotoa huduma za dharura kama ambulensi zikipata wakati mgumu kupita katika barabara hizo.

Siku chache kabla ya sherehe za Pasaka, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kusitishwa kwa shughuli zote za usafiri na matembezi ndani ya jiji la Nairobi na majimbo mengine, kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri , kama hatua ya kudhibiti mlipuko wa maambukizi ya COVID-19 nchini.

Polisi waliondoa vizuizi vya barabarani saa kadhaa baadae, kuwaruhusu watu kwenda nyumbani.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *