img

Ufaransa yawataka watu kutoka nchi kadhaa kukaa karantini

April 18, 2021

 

Ofisi ya Waziri Mkuu nchini Ufaransa imetangaza kuwa nchi hiyo itaweka masharti kwa watu wanaowasili nchini humo kutoka Argentina, Brazil, Chile na Afrika Kusini kukaa karantini ya lazima kwa siku 10 kufuatia wasiwasi wa aina mpya ya kirusi cha corona.

Ofisi hiyo hata hivyo imesema ndege kutoka mataifa hayo hazitapigwa marufuku, lakini abiria wanaotokea nchi hizo watatakiwa kukaa karantini la sivyo wakabiliwe na faini.

Ufaransa imetetea uamuzi wake wa kutopiga mafuruku safari za ndege kutoka mataifa matatu ya Argentina, Chile na Afrika Kusini kwa kusema aina mpya ya kirusi kilichopatikana katika nchi hizo haijafikia kiwango cha kutisha kama kilichoshuhudiwa nchini Brazil.

Hatua hizo mpya za karantini zitaanza kutekelezwa hatua kwa hatua katika siku zijazo hadi zitakapotekelezwa kikamilifu kufikia Jumamosi ijayo.

Hivi karibuni, Ufaransa iliimarisha vikwazo vyake vya kupambana na wimbi la tatu la virusi vya corona.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *