img

Sheffield United yashuka daraja ikiwa na mechi mkononi

April 18, 2021

WILLIAN Jose, nyota wa Wolves atabaki kwenye kumbukumbu ya wachezaji wa Klabu ya Sheffield United kwa kuwa aliwatungua bao pekee la ushindi lililowashusha daraja.

Mchezo huo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Molineux,  Sheffield United ilipiga jumla ya mashuti mawili yaliyolenga lango huku Wolves wakipiga matano na moja kati ya hayo ni lile lililopigwa na  Jose dakika ya 59.

Sheffield United ilikuwa inahitaji ushindi  kwenye mchezo huo ili kujiepusha na hatari ya kushuka daraja licha ya kutengeneza nafasi ilikuwa ngumu kwao kufunga jambo ambalo limewagharimu.

Kupitia Ukurasa wao rasmi wa Instagram,  Sheffield United inayonolewa na Kocha Mkuu, Paul Heckingbottom wamesema kuwa kupoteza katika Uwanja wa Molineux kumefanya safari yao ndani ya Ligi Kuu England kufika ukingoni.

Sasa Sheffield United itashiriki Championship kusaka nafasi ya kurudi tena ilikotoka kwa kuwa msimu huu imekusanya jumla ya pointi 14 baada ya kucheza jumla ya mechi 32.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *