img

Ramadhan: Fahamu vyakula ambavyo waliofunga wanastahili kula au kutokula

April 18, 2021

Dakika 13 zilizopita

Mboga na matunda

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi ambacho waumi wa dini ya Kiislamu hufunga kuanzia alfajiri hadi jioni ikitegemea na mahali ulipo.

Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan ni tendo la ibada, ambalo linawawezesha Waislamu kujiweka karibu na Mungu na kuimarisha imani yao ya kidini.

Hata hivyo, mbali na hayo, ni kipindi ambacho watu hujikuta wakila aina nyingi ya vyakula wakati wanapofungua mfungo.

Lakini je, unajua ni aina gani ya vyakula mtu aliyefunga anastahili kula?

Waathirika wa vyakula fulani

Kulingana na Dkt. Lawan Musa Tahir, wa mjini Abuja kwanza kuna wale ambao pengine ni wagonjwa wa kisukari au wenye maradhi ya ini, wanastahili kuendelea kuzingatia vyakula vyao.

Hali hii ni sawa na yeyote mwenye tatizo na chakula fulani, pengine miili yao hudhurika wanapokula vyakula fulani, hata kama umefunga mwezi wa Ramadhani, unapofungua zingatia vyakula vyako vya kila siku.

Pia kuna mazingira tofauti ya kuishi, kuna wale wanaoishi maeneo ya jua kali ambako watu wanakunywa maji mara kwa mara. Wanapofungua wajitahidi kunywa maji kwa wingi.

  • Orodha ya vyakula ambavyo waliofunga wanastahili kula au kutokula:
  • Epuka vyakula vyenye viungo vingi na mafuta mengi kwasababu vitaongeza kiu na joto mwilini
  • Kula vyakula vyenye majimaji hasa matunda kama vile, ndizi, nanasi, papai, matikiti maji na kadhalika
  • Kunywa maji moto kama vile chai, kakao kwasababu inatayarisha tumbo baada ya kukaa saa nyingi bila kula chakula
  • Epuka kujaza tumbo chakula – utaona kuna watu wanaokula kupita kiasi wakati mmoja. Hilo ni tatizo. Ikiwa utafanya hivyo, mwili wako hauwezi kutumia vizuri ile nguvu au nishati ya mwili ambayo umepata kwa wakati mmoja. Hili linaweza kusababisa kuongeza uzito. Ni vyema kula kidogo kidogo kisha unapumzika ili uweze kula tena baadaye
  • Pia usivute sigara unapokuwa karibu na jamaa zako kwasababu ni hatari kwa afya
  • Hakuna tatizo lolote na kufanya mazoezi wakati wa mfungo – lakini fanya kidogo kidogo
  • Matunda yaliyokauka kama vile tende, lozi na jozi pia ni muhimu sana kupata. Zina uwezo wa kukufanya uhisi umeshiba kwa kipindi kirefu cha siku.

Unapofunga mwezi wa Ramadani, sio tu kwamba unabadilisha mfumo wako wa kula bali pia mfumo wa kulala, na pia utakuwa katika mabadiliko ya kimwili na kisaikolojia.

Pia ni vyema kufahamu kuwa mwili kutokuwa na maji ya kutosha na kukosa kula kwa wakati kama ulivyozoea, kasi ya umeng’enyaji wa chakula inapungua ili kutumia nguvu ulio nayo kwa ufasaha zaidi.

Ni wazi kwamba kipindi cha mfungo wa Ramadhani kama hiki, sio tu suala la chakula utakachokula, lakini pia kiwango cha chakula na aina ya chakula unachokula, kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha mwili unakuwa na afya njema kila wakati.

Na ili kuwa na nguvu na virutubisho vinavyohitajika mwilini kila siku, unastahili kula vyakula vyenye protini, wanga, vitamini na madini mengine, na pia unastahili kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *