img

Yuri Gagarin:Hatari fiche zilizomkabili mwanadamu wa kwanza kwenda anga za mbali

April 17, 2021

Dakika 5 zilizopita

Yuri Gagarin wearing a space helmet

Chanzo cha picha, Getty Images

“Nimeketi kwenye kopo la bati, juu kabisa ya dunia. Ulimwengu ni rangi ya buluu na hakuna ninachoweza kufanya.”

Mashairi hayo kutoka kwa wimbo ‘Space Oddity’ wa David Bowie unaangazia kwa ujumla namna Yuri Gagarin alivyohisi wakati amefunga safari ya kwanza kwa mwanadamu kwenda anga za mbali.

Katika chombo chake kidogo, chenye kipenyo cha mita mbili pekee, Gagarin alifunga safari ya kwenda anga za mbali zaidi akiwa kama msafiri tu badala ya mwanaanga.

Wakati huo, “rubani” hata hakukugusa vidhibiti vya chombo kilichotumika.

Kulingana na mawasiliano yaliyokuwepo na wadhibiti kwenye ardhi, Gagarin alishikwa na mshangao baada ya kuona muonekano aliokutakana nao kupitia madirisha ya chombo alichokuwa anatumia, huku akisema dunia yetu kwa ujumla ni nzuri hasa vivuli vya mawingu juu ya ardhi.

Safari ya Gagarin kwenda anga za mbali Aprili 12, mwaka 1961 ulikuwa ushindi mkubwa kwa Muungano wa Usovieti katika ushindani wake dhidi ya Marekani na kurejea kwa mwanaanga huyo duniani ilikuwa furaha isiyo kifani kwao.

Lakini ili kuweka historia, Gagarin aliamua kufanya jambo lililokuwa hatari kweli na lilihitaji ujasiri wa hali ya juu. Aliamua kwenda anga za mbali – eneo ambalo hakuna wakati huo aliyekuwa amewahi kufika – kwa kutumia chombo ambacho hakikikuwa na vidhibiti vyovyote vya uokozi.

Wakati huo huo, roketi ambayo ingemuongoza katika safari hiyo, ilikuwa imewahi kufanikiwa na pia kushindwa kufanyakazi kama ilivyotarajiwa katika baadhi ya safari.

Gagarin aliamua kuchukua jukumu la kuwa majaribio katika safari hiyo ya anga ambayo ilikuwa imepangwa kujibu maswali kadhaa. Je mwanadamu anaweza kuishi akiwa kwenye anga la mbali? Na je chombo hicho cha kwenda anga za mbali kinaweza kuwasiliana sawasawa kikiwa ardhini ili kuhakikisha kwamba anatua salama?

Wakati huo, hakuna aliyekuwa anaamini usalama wa roketi, chombo kinachotumiwa kwenda anga la mbali, mifumo na vidhibiti vya mawasiliano – au hata ikiwa mwanadamu anaweza kuishi katika anga za mbali.

“Ikiwa chombo cha Vostok leo hii kingepewa wanasayansi, hakuna ambaye angakubali kwenda nacho anga za mbali,” amesema mhandisi Boris Chertok karibu nusu karne baada ya safari hiyo, katika kitabu chake cha ‘Roketi na Watu’.

“[Wakati huo] Nilitia saini nyaraka zilizoonesha kuwa kila kitu kiko sawa kwangu na nikatoa hakikisho la usalama kwa safari za aina hiyo. Lakini nisingeweza kutoa hakikisho kama hilo hii leo. Nimepata tajriba ya kutosha na nimegundua kwa kiasi gani tuliweka maisha hatarini.”

Mapungufu ya Vostok

Kuanzishwa kwa roketi ya Vostok, ambapo chombo kilichopewa jina hilo hilo kiliwekwa kwenye roketi ya R-7, kombora lenye uwezo wa kufika bara jingine ambalo safari yake ya kwanza ilikuwa ni Agosti mwaka 1957.

Mwaka huo huo, Sputnik 1, setelaiti ya kwanza bandia duniani ilitokana na R-7.

Vilivyoundwa kutokana na R-7 vilijitokeza kuwa na mafankio makubwa – makombora yalitokana na roketi hii nchini Urusi bado ndio pekee yanayotumika kwa ajili ya safari za anga za mbali. Ingawa mambo yamebadilika, imejidhihirisha kuwa thabiti kwa uwasilishaji wa chombo cha anga kwenye mzingo.

Hata hivyo, mwaka 1961, mambo yalikuwa tofauti.

Close-up of the exhaust flames of the rocket launching Yuri Gagarin into orbit

Chanzo cha picha, Science Photo Library

“Tukiangazia viwango vya sasa hivi vya usalama wa roketi, kama kulikuwa na mwaka wenye matumani ni 1961. Mwaka huo, kulikuwa na urushaji wa karibu roketi nane kufuatana na moja pekee ndio ambayo ilitua kwa namna ya kawaida.”

“[Lakini] kati ya roketi 5 zilizorushwa mwaka 1960, nne zilitua kando ya ardhi, na kati ya hizo, tatu zikafanikiwa kutoka kwenye mzingo wa dunia na mbili pekee ndizo zilizotua. Na kwa mbili zilizofanikiwa kurejea a kurushwa katika mpango wa Vostok ilikuwa ni Mei 15, mwaka 1960 – chini ya mwaka mmoja kabla ya safari ya Gagarin. Miongoni mwa chombo hicho ilikuwa ni roboti iliyopewa jina la Ivan Ivanovich.

Chombo hicho kilifanikiwa kuondoka kwenye mzingo wa dunia lakini haikurejea tena kwasababu mifumo yake ilifeli na kushindwa kufanya kazi.

Agosti 19, mbwa Belka na Strelka walikwenda anga za mbali na kurejea na kufanya safari hiyo kuwa pekee iliyofanikiwa kwa mwaka 1960.

Lakini majaribio mafanikio yake yalikuwa kidogo sana.

Desemba 1, kukawa na jaribio la safari nyingine ambapo pia mbwa Mushka na Pchelka walibebwa – lakini hawakurejea katika njia ambayo walitarajiwa na kuanza kushuka nje ya mipaka ya Umoja wa Kisosvieti.

Chombo chote kiliharibika ikiwemo wanyama waliokuwa ndani ili kuzuia nchi zingine zisifanikiwe kunasa teknolojia ya Umoja wa Kisovieti.

Vyombo vilionekana kuwa sawa

Wakati wa safari ya Gagarin Aprili 12 mwaka 1961, roketi zilifanyakazi sawasawa.

Lakini hakuna jambo dogo katika teknolojia ya anga za mbali na hilo nusra limgharimu Gagarin maisha yake.

Miongoni mwa changamoto alizokumbana nazo ni chombo chake kuingia katika mzingo kikiwa katika mwinuko wa juu zaidi kuliko ilivyokadriwa.

Walishika breki lakini kama hazingefanya kazi, Gagarin angelazimika kungoja chombo chake kianze kurejea chenyewe duniani.

Ingawa chombo Vostok kilikuwa na oksijeni, chakula na maji vya muda wa wiki moja, kuwa na mwinuko wa juu kungefanya chombo hicho kichukuwe muda mrefu zaidi kuanza kurejea.

Na hilo, bila shaka lingemfanya Gagarin kukosa chakula na angefariki dunia tu. Kwa bahati nzuri breki zilifanya kazi vizuri.

Steam rising from chimneys plant near a monument of Yuri Gagarin, during sunset in Moscow

Chanzo cha picha, Reuters

Kebo ambazo zilikuwa zinaunganisha chombo hicho na moduli ya kutoa huduma, vilishindwa kutengana kabla ya Gagarin kurejea duniani. Kwahiyo, chombo cha Gagarin ghafla kikawa na mzigo wa kubeba moduli ya ziada wakati kinatua.

Pia kiwango cha nyuzi joto kwenye chombo kilikuwa cha juu sana kiasi cha kuhatarisha maisha na Gagarin akawa anazunguka kweli mduara kwa kasi ya juu karibu apoteze fahamu.

“Ilikuwa ni wingu la moto linalokimbia duniani,” mwanaanga huyo baadaye alianza kukumbuka kilichotokea. Ilikuwa ni dakika 10 kabla ya kebo hatimaye kuungua kabisa na moduli ya kushuka yenye binadamu kuwa huru.

Gagarin alitoka kwenye chombo kabla hakijatua ardhini na kutumia parachuti kutua salama karibu na mto Volga.

Hilo lilikiuka masharti yaliyowekwa na Shirikisho la Anga Kimataifa kwamba wanaanga wote wanastahili kutua katika chombo chao, la sivyo, safari yao huenda isitambulike.

Maafisa walikataa kukubali kwamba safari ya Gagarin haikubaliki.

Rekodi ya safari yake iliidhinishwa na Shirikisho la Anga Kimataifa ambayo pia ilibadilisha sheria zake na kukubali kwamba hatua muhimu kabisa ni kutua salama na kurejea kwa rubani.

‘Nimepata tajriba ya kutosha’

Mwanahabari wa BBC Urusi alimuuliza mwanaanga wa Urusi ikiwa anaweza kusafiri kwa kutumia chombo cha Vostok jinsi kilivyokuwa mwaka 1961.

Pavel Vinogradov, ambaye alisafiri anga la mbali mara tatu mwaka 1997, 2006 na 2016, alisema kwamba angeweza kusafiri licha ya hatari zilizopo kwasababu ya sifa yake ya kutaka kujua kitakachotokea.

Hata hivyo, Gagarin alikuwa katika nafasi nyengine tofauti, anasema, na huenda hakujua hatari zote zilizomkabili.

“Lazima uelewe kuwa mara yangu ya kusafiri anga la mbali,” anasema Vinogradov. “Mimi ni mhandisi, Najua mengi. Gagarin, pengine, hakujua hayo yote.”

Mikhail Kornienko, ambaye anasema alisafiri kwenda anga za mbali mwaka 2010 na 2015, anasema kuwa bila shaka safari ya mwaka 1961, kama angekuwa Gagarin, lakini ikiwa ni wakati huu hangethubutu kwenda kwasababu hatari iliyokuwepo imetambulika kuwa ya juu mno.

“Nina uhakika hakuna ambaye angethubutu kwenda kwa kutumia chombo hichi,” mwanaanga huyo amesema.

Badges featuring Yuri Gagarin

Maisha yetu yalibadilika kabisa’

Kijana wa mkulima Gagarin alikwenda anga la mbali kwa mara ya kwanza na kurejea akiwa mtu maarufu kabisa duniani.

Safari yake ilimfanya kuwa shujaa na mashhuri kote dunia na baada ya hapo alisafiri kwingi kutangaza mafanikio ua Umoja wa Usovieti – ikiwemo Czechoslovakia, Bulgaria, Finland, Uingereza, Iceland, Cuba, Brazil, Canada, Hungary, na India.

“Bila shaka ilimaanisha kuwa maisha yetu yamebadilika kabisa,” amesema Elena Gagarina, alipozungumza na BBC mwaka 2011

“Ilikuwa vigumu sana kwa wazazi wangu kuwa na maisha ya faragha tena.

Na ingawa Gagarin alitamani kwenda tena katika anga za mbali, alipigwa marufuku kwasababu ya hadhi yake kama shujaa wa taifa.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *