img

Waliokufa kwa Covid-19 wapindukia watu milioni 3 duniani kote

April 17, 2021

Idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 duniani kote leo hii imepindukia milioni tatu. Idadi hiyo ni kwa mujibu wa majumuishi yaliofanywa na shirika la habari la Ufaransa AFP, huku idadi ya vifo ikitajwa kuendelea kuongezeka pamoja na uwepo wa kampeni za utoaji chanjo.

Baada ya kupatikana kwa unafuu kidogo kwa mwezi uliopita, idadi ya vifo vya kila siku imekuwa ikiongezeka, kwa wastani wa vifo 12,000 kwa siku juma lililopita. 

Wakati nchi zingine kama Israel zimeonekana kunufaika na jitahada za utaoji chanjo kwa umma wa watu nyingine kama India zinapambana na hali ya kuongezeka kwa maambukizi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *