img

Somaliland na Taiwan: Maeneo mawili yenye marafiki wachache

April 17, 2021

Dakika 6 zilizopita

Mohamed Hagi (R), Somaliland's Taiwan representative, bumps elbows while posing with Taiwan's Foreign Minister Joseph Wu during the opening ceremony of the Somaliland representative office in Taipei on September 9, 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Ubalozi wa Somaliland ulifunguliwa Taiwan mwezi Septemba mwaka jana

Taiwan na Somaliland ni maeneo mawili ambayo yote yanajitegemea kikamilifu ambayo yalijitangazia uhuru wake lakini hakuna ambalo linatambuliwa kimataifa na sasa hivi inasemekana kuwa yanaendelea kuwa na uhusiano wa karibu.

Bendera ya Taiwan inapepea katika upepo mwanana kwenye ubalozi wao huko Somaliland- yenye rangi nyekundu, nyeupe na buluu kwenye anga angavu ya buluu.

Ingawa kuna baadhi ya watu wanaoona uhusiano wao kama usio wa kawaida, Somaliland na Taiwan zina uhusiano wa karibu.

Zinakasirisha China na Somali

Maeneo yote mawili hayatambuliwi kimataifa na yote yana majirani wakubwa – Somalia na China – ambazo zinasisitiza kuwa maeneo hayo ni sehemu yao.

Somaliland na Taiwan walianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka jana kutokana na hasira iliyosababishwa na hao majirani zao.

Somalia iliishutumu Taiwan kwa kuwa marafiki na Somaliland. Maafisa wa China walisafiri hadi Somaliland na kusisitiza kuwa ikate uhusiano wake wa karibu na Taiwan.

Kuna uwezekano mkubwa China inachukulia uhusiano wa Taiwan na Somaliland kama kivurugi cha mradi unaofahamika kwa jina ‘Belt and Road Initiative’, wenye mpango wa kujenga barabara za kibiashara baharini na ardhini kote Asia, Mashariki ya Kati na Afrika.

Somaliland inayoonekana kama kizuizi yenye bandari yake ya kimkakati ya Berbera, huenda ikazuia ujenzi wa barabara yake ya kibiashara katika eneo la mashiriki mwa pwani ya Afrika.

Allen Chenhwa Lou

BBC

Somaliland is Taiwan’s gateway to East Africa, from here I represent Taiwan in 10 East African countries”

1px transparent line

China pia huenda inachukulia uhusiano wa Somaliland na Taiwan kama wa kutiliwa mashaka kidogo kwasababu imeanzisha kambi zake za kijeshi kwa mara ya kwanza duniani, nchi Jirani ya Djibouti.

Taiwan inaichukulia Somaliland kama hatua ya kwanza ya kutimiza ndoto zake eneo hilo.

“Somaliland ni lango la kibiashara la Taiwan kuingia Afrika Mashariki,” amesema mwakilishi wa Taiwan eneo la Somaliland, Allen Chenhwa Lou.

“Kuanzia hapa nawakilisha Taiwan katika nchi 10 za Afrika mashariki ikiwemo Kenya na Ethiopia.”

Somaliland ni moja ya maeneo mawili tu ya Afrika kuwa na uhusiano uliokamilika wa kidiplomasia na Taiwan. Ya kwanza ilikuwa ni taifa la Eswatini ambazo zilianzisha uhusiano wao mwaka 1968.

‘Kaka mkubwa wa Somaliland’

Bwana Lou anaelezea uhusiano kati ya maeneo hayo mawili kama ushindi kwa pande zote.

Taiwan inatoa usaidizi katika nyanja za kilimo, teknolojia, elimu, afya, uchaguzi na nishati. Somaliland pia ipo eneo la kimkakati, yenye utajiri wa samaki, mali asili na uwezo wa kunawiri katika utalii.

“Somaliland inaita Taiwan ‘kaka mkubwa’,” amesema Bwana Lou. “Lakini napendelea kuona uhusiano wetu uwe ni wenye ushirikiano zaidi na kushirikishana. Daima tutakuwa pamoja na Somaliland.

“Hatuna haja ya kutafuta uhuru wetu kwasasa kwasababu tayari tuko huru. Kile ambacho sote tunahitaji ni kutambulika. Sote tunapitia hali hii ngumu.”

Presentational grey line

Somaliland Somalia

A Russian made mig fighter jet that was used in 1989 seen hanging in Hargeisa as a monument of reminder to the people of Somalilan

Chanzo cha picha, AFP

  • Walikuwa wakitawaliwa na Uingereza na ilijiunga na eneo jingine la Somalia Julai 1 mwaka 1960
  • Ikatangaza uhuru wake baada ya kung’olewa madarakani kwa aliyekuwa dikteta wa Somalia Siad Barre mwaka 1991
  • Hatua hiyo iliwadia baada ya mapigano ambapo makumi ya maelfu ya watu waliuawa na kutoroka miji yao
  • Somaliland ina mfumo wake wa kisiasa, taasisi zake za serikali, kikosi cha polisi na pia ina sarafu yake
Presentational grey line

Lakini sio kila mmoja huko Somaliland anafurahia uhusiano wa pande hizo mbili huku wengine wakifikiria kupoteza China kama mshirika sio jambo la busara.

“Watu wawili wasiokuwa na lolote hawawezi kusaidiana,” amesema mfanyabisahara wa mifugo Ismail Mohamed. “Tunahitaji China yenye nguvu zaidi kuliko Taiwan.”

Mfanyabiashara mwanamke Muna Aden ana mashaka.

“Uhusiano na Taiwan unaonesha wendawazimu wa raia wa Somaliland,” amesema.

“Tulifikiria kuwa Somaliland iligeukia Taiwan kama njia moja ya kujaribu kuvutia China na kusema: ‘Ikiwa hamutatuoa, tutaolewa na yule mwingine’. Hatukuwahi kufikiria wanaweza kuwa na uhusiano wa karibu.

“Ni makosa makubwa sana ambayo China haiwezi kusahau.”

Lakini mamlaka ya Somaliland inatetea uhusiano huo huku Waziri wa mambo ya nje Liban Yousuf Osman, akisema maeneo hayo mawili wamekuwa na maadili yanayofanana ya demokrasia a uhuru.

“Tunakaribisha nchi yoyote ambayo inataka kuwa na uhusiano na Somaliland ikiwemo China. Lakini hatutafukuza Taiwan kwasababu ya China.”

Presentational grey line
  • China na Taiwan zimekuwa na serikali tofauti tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini China mwaka 1949
  • Wasiwasi umekuwa ukiongezeka miaka ya hivi karibuni na Beijing haijaondoa uwezekano wa kutumiaji nguvu kuchukua tena kisiwa hicho
  • Ingawa Taiwan inatambulika rasmi na nchi kidogo tu, serikali yake iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ina uhusiano thabiti wa kibiashara na usio rasmi na nchi nyingi
Presentational grey line

Kwa upande wake, Somaliland imefungua milango yake kidiplomasia na Taiwan ikiongozwa na Mohamed Hagi.

“Nafurahia sana kuishi hapa Taipei,” anasema.

“Nimeelezea kuwa Somaliland sio Somalia, ambayo wanaihusisha na maharamia na ugaidi.”

Bwana Hagi anasema anachojua yeye ni kwamba, wako raia watatu wa Somaliland eneo la Taiwan – yeye mwenyewe na wengine wawili anaofanya nao kazi.

Lakini pia anatarajia idadi hiyo kuongezeka karibuni kwasababu wanafunzi 20 kutoka Somaliland wamepewa ufadhili wa masomo na Taiwan na kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa wafanyabiashara huku ushirikiano wa kiuchumi ukiendelea kuimarika.

Mwakilishi wa Taiwan naye huko Somaliland Bwana Lou anaelezea vile ambavyo watu wa Somaliland walifikiria anatoka China, huku akipatwa na mshutuko wa kiutamaduni wakati anawasili eneo hilo mwaka 2020 kwasababu ilikuwa mara yake ya kwanza kufika Afrika.

Map
1px transparent line

“Napenda sana kutembea mitaani. Kila mmoja alikuwa akiniangalia na kusema: ‘Ni Mchina’. Na mimi sikusita kuwaarifu kwamba: ‘Hapana. Mimi ninatoka Taiwan’.” Amesema Bwana L

“Lakini pia bado kuna mengi yanayohitaji kufanyika,” Bwana Lou amesema.

“Nilikuwa ufuoni msichana mdogo akaja huku wengine wakimfuata. Akaanza kuniotesha kidole na kupiga kelele akitaja jina ‘Covid-19!’. Kwa mara nyingine tena nikalazimika kusema: ‘Hapana, mimi ninatoka Taiwan’, lakini sina uhakika kama alinielewa kwasababu alikuwa anazunguza Kisomali pekee.”

Ingawa bado ni mapema mno kusema ikiwa urafiki wa maeneo hayo mawili utasaidia pande zote mbili na hasa kutimiza kiu yao ya kutaka kutambulika, au kama uhusiano wao utakuwa ni wenye kuchokoza China na Somalia kwa kiasi gani.ou.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *