img

Sayansi ya mazungumzo inavyoboresha mahusiano yenu ya kimapenzi

April 17, 2021

 

Kuna uhusiaono mkubwa kati uzungumzaji wako na mpenzi wako katika kuyafanya mahasiano yenu yawe matumu zaidi. Unavyozungumza na mpenzi wako ni tofauti kabisa na unavyozungumza na watu wengine. Ni hatari sana kutumia lugha ya ukali ama isiyo ya kiungwana kwa mpenzi wako.

Unatakiwa kufahamu kwamba, mpenzi wako ni mtu muhimu sana katika maisha yako hivyo unatakiwa kuwa makini pindi unapozungumza naye.

Kuonesha kwamba wapo wasiojua mapenzi ni nini, unamkuta mtu anamwita mpenzi wake majina kama vile mshamba, demu, shembe na mengine mengine kama hayo. Mpenzi wako kweli umuite demu? Na wale wengine kule mtaani utawaita nani?

Huo si ustaarabu na kamwe mapenzi yenu hayawezi kushamiri kwa mtindo huo. Kuna wengine matusi hayawaishi midomoni mwao. Kwa kufanya hivyo jua tu kwamba unamboa laazizi wako.

Aidha mapozi katika uzungumzaji wako ni miongoni mwa vitu vinavyoweza kumdatisha mpenzi wako. Ukiwa na mpenzi wako usiongee kama chiriku au kama unagombana na mtu. Ongea kwa mapozi na hilo litamfanya akutofautishe wewe na watu wengine.

Kuna ambao wanapozungumza na wapenzi wao hawapitishi sentensi bila kutaja neno Dear ama Sweet. Hakika inavutia na ni mbolea tosha katika penzi la watu hao.

Lakini pia kuna baadhi ya maneno ambayo ukiyafanya kuwa sehemu ya maisha yako yanaweza kumvutia mpenzi wako. Kwa mfano neno NAKUPENDA!

Hakuna asiyefurahia kupendwa hata kama ni mtoto mdogo, anafurahi sana kusikia neno ‘Nakupenda’ kutoka kwa watu wake wa karibu. Lakini linapokuja suala la mahusiano ya kimapenzi, neno hilo linachukua nafasi kubwa sana.

Ili kulifanya neno hilo kuwa na uzito wengine hulitamka kwa lugha ya kigeni yaani ‘I love you Dear au sweet’, ni sawa tu kwani maana ni ile ile. Huo ni mfano wa maneno ambayo ni chachu katika mapenzi.

Pia unatakiwa kuwa mwepesi wa kushukuru. Wengine hata wapenzi wao wajitahidi kuwafanyia mambo mazuri vipi, lakini ni wagumu sana kutamka neno ASANTE.

Hata wanapowakosea wapenzi wao ni wagumu sana kuomba samahani. Kwa taarifa yako kama wewe ni mmoja wa wenye tabia hiyo elewa kwamba unamboa sana mpenzi wako.

Pia mnapokuwa faragha na mpenzi mkistarehe,baada ya kukufanyia kile ambacho roho yako imefurahi, mwambie asante kwa kukupeleka kwenye sayari mpya ya mahaba.
,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *