img

Rais wa Marekani Joe Biden apuuza ahadi yake ya kuwaruhusu wahamiaji wengi kuingia nchini humo

April 17, 2021

Dakika 7 zilizopita

Ikulu ya White House imesema kwamba rais Biden ataongeza idadi hiyo mwezi ujao

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Katika hotuba aliyotoa mnamo Februari, Bwana Biden aliapa kuongeza idadi hiyo hadi 125,000 katika mwaka ujao wa bajeti.

Rais wa Marekani Joe Biden amebadilisha mawazo muda mfupi baada ya kusaini agizo linalothibiti idadi ya wahamiaji wanaoruhusiswa kuingia marekani kusalia kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Donald Trump .

Bw Biden alizua hamaki ya wengi siku ya ijumaa alipoacha idadi hiyo kusalia watu 15,000 kwa mwaka miezi miwili tu baada ya kuahidi kwamba angeongeza idadi ya wahamiaji wanaoruhusiswa kuingia Marekani kufika watu 65,000 .

Ikulu ya White House imesema kwamba rais Biden ataongeza idadi hiyo mwezi ujao . Ripoti zasema Biden anahofia kuwaacha wakimbizi wengi kuingia nchini humo hasa baada ya idadi kubwa kujitokeza katika mpaka wa Marekani na Mexico .

Takwimu za umoja wa mataifa zaonyesha kwamba kuna zaidi ya wakimbizi milioni 80 kote duniani huku asilimia 85 wakipewa makao na mataifa yanayostawi .

Amri ya Biden ilifanya nini?

Ikulu ya White House ilisema agizo la Ijumaa litaongeza kasi ya usajili wa wakimbizi wanaoingia Marekani – tangu Oktoba karibu watu 2,000 wamesajiliwa chini ya mpango huo.

Amri hiyo pia inabadilisha ugawaji wa nani anaruhusiwa kuingia, na nafasi zaidi zinapewa wanaowasili kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kati, na kukomeshwa kwa vizuizi juu ya watu wapya wanaotaka kuingia Marekani kutoka Somalia, Syria na Yemen.

Lakini Bwana Biden – ambaye aliapa kuongeza kiasi cha idadi ya juu ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia Marekani wakati wa kampeni yake – aliweka idadi kubwa zaidi inayoruhusiwa kila mwaka kufikia 15,000, kiwango kilichowekwa na mtangulizi wake Donald Trump.

Bwana Biden alisema kiwango hicho cha enzi ya Trump “bado kinakubaliwa kwa sababu ya wasiwasi kuhusu hali ya kibinadamu na ni kwa masilahi ya kitaifa”.

Ikulu ilisema nini baadaye?

Msemaji wa Ikulu, Jen Psaki alisema agizo la rais huyo wa chama cha democrat lilikuwa “jambo la kuchanganya” baada ya habari hiyo kuzua ghadhabu kati ya makundi ya misaada, na pia kutoka kwa chama cha Bw Biden. Mwenyekiti wa kamati ya Masuala ya Kigeni wa Seneti Bob Menendez alielezea kwamba idad hiyo ni ya chini sana kwa kiwango cha ‘kushangaza “.

Bi Psaki alisema kwa Bw Biden ameshindwa kutekeleza ahadi yake ya kuruhusu wakimbizi u 62,500 ambayo alitangaza kwa Bunge miezi miwili iliyopita kwa sababu ya ‘mfumo dhaifu wa kuwasajili wakimbizi’ waliorithi kutoka kwa utawala wa hapo awali

Bi Psaki alisema agizo la Bw Biden Ijumaa lilikuwa na dhamira ya kuruhusu ndege za wakimbizi kwenda Marekani kuanza ndani ya siku chache.

Aliongeza kusema : ” Baada ya hilo kufanyika tunamtaraji rais kuweka idadi ya mwisho iliyoongezwa ya wakimbizi kwa muda uliosalia wa mwaka huu wa kifedha kufikia mwezi Mei tarehe 15′

Young migrants at the crowded facility in Donna are separated by plastic sheeting

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wakimbizi wa umri mdogo waliozuiliwa katika kituo kimoja huko Donna

Hakusema idadi hiyo ingawaje aliongeza kwamba lengo lake lake la kuwaruhusu wakimbizi 65,000 huenda lisiweze kutimizwa

Katika hotuba aliyotoa mnamo Februari, Bwana Biden aliapa kuongeza idadi hiyo hadi 125,000 katika mwaka ujao wa bajeti.

Karibu wakimbizi 85,000 walipewa makazi yao huko Marekani katika mwaka wa mwisho wa rais Barack Obama.

Je,Watu wamechukuliaje mabadiliko hayo?

Jenny Yang, makamu wa rais mwandamizi wa Shirika la Word Relief , shirika la kutoa msaada wa kibinadamu, aliiambia CNN kwamba White House inadai kwamba mpango wa makazi ya wakimbizi wa Marekani unahitaji kuundwa upya baada ya miaka ya Trump kuwa “hadithi ya uongo kabisa”.

“Haijasimama katika ukweli wowote,” alisema. “Sio kwamba hawana rasilimali. Ni hesabu ya kisiasa wakati huu.”

Afisa mmoja wa Marekani mapema aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba utawala wa Biden ulikuwa na wasiwasi juu ya kuonekana “wazi sana” huku pakiwa na idadi inayoongezeka ya wahamiaji wanaowasili katika mpaka wa Mexico.

Mnamo mwezi Machi takribani wakimbizi 172,000 walisimamishwa katika mpaka wa Marekani na Mexico -idadi ya juu sana katika miaka 20 – na wengi walikuwa watoto ambao hawakuwa na watu wazima kuwalinda .

Mwandishi wa hotuba za Trump na mshauri wake kuhusu masuala ya uhamiaji Stephen Miller aliandika katika twitter kama uamuzi huo wa Biden ulionyesha kwamba kundi la Biden lilifahamu hatari ya kuwaruhusu wakimbizi kufurika Marekani na huenda chama cha rais wa sasa kingeshindwa katika uchaguzi wa kati kati ya muhula ambao utafanyika Novemba mwaka wa 2022

Agizo hilo la Biden liliwachukiza wanachama wengine wa chama cha Democratic .

Mwakilishi wa bunge wa New York Alexandria Ocasio-Cortez aliandika katika twitter : ‘Kuzitumia sera za ubaguzi wa rangi za Trump na washirika wake ni jambo linaloturejesha chini sana kihistoria ,kuacha idadi hiyo kusalia ilivyo ni jambo baya .Timiza ahadi yako’

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *