img

Prince Philip: Malkia aitoa kwa umma mojawapo ya picha zake anazozithamini

April 17, 2021

17 Aprili 2021, 14:51 EAT

Imeboreshwa Dakika 4 zilizopita

The Duke of Edinburgh and the Queen, pictured in the Scottish Highlands in 2003

Chanzo cha picha, Countess of Wessex via Press Association

Malkia Elizabeth ameitoa kwa umma moja ya picha zake anazozipenda sana akiwa pamoja na mume wake wa miaka 73 , Mtawala wa Edinburgh, katika siku ya mazishi yake.

Wanandoa hao wa ufalme wa Uingereza walipigwa picha hiyo wakiwa wamepumzika kwenye majani katika eneo zuri la Aberdeenshire katika picha iliyochukuliwa na mkuu wa kaunti ya Wessex mwaka 2003.

Philip anaonekana akiwa amelala nyuma, huku akiwa ameegemea kiwiko, huku kofia yake ikiwa imetundikwa kwenye goti lake.

Mazishi yake yatafanyika katika kasri la kifalme la Windsor Castle saa tisa kwa saa za Uingereza(15:00 BST) Jumamosi.

Watoto wa Mtawala huyo watatembea nyuma ya jeneza lake wakati wa matembezi ya kuusindikiza mwili wake.

Katika picha hiyo iliyopigwa katika siku iliyokuwa ya jua karibu na mji wa Aberdeenshire wa Ballater, Malkia na Mwanamfalme Philip walionekana watulivu na walimtazama kwa tabasamu mkwe wao Sophie ambaye alipiga picha hiyo.

Malkia – alikua amevalia sketi, blauzi na sweta pamoja na shanga shingoni-huku wakiwa wameketi na mume wake.

Wakati huo huo , Mike Tindall, ambaye amemuoa mjukuu wa Malkia na Mwanamfalme Philip Zara Tindall, ametoa salamu zake za rambi rambi kwa baba mkwe wake Mtawala wa Edinburgh ambaye amemtaja kama “mwanaume aliyejitolea kwa familia yake ambaye hatakumbukwa tu bali atakayependwa daima “.

Mchezaji wa zamani wa timu ya raga ya Uingereza alituma picha kwenye mtandao wa Instagram kutoka katika albamu ya picha za kibinafsi ya Familia ya ufalme ya Mwanamfalme Philip akiwa pamoja na mtoto mkubwa wa kike wa Tindall Mia.

Presentational white space

Picha hiyo iliyochukuliwa na Wanamfalme wa Cambridge, inamuonesha Mia na babu yake mzaa baba wakila chakula pamoja kwenye benchi mbele ya nyumba ndogo iliyojengwa kwa mbao.

Nusu glasi ya bia inaonekana nyuma ya Mwanamfalme upande wa mkono wake wa kulia.

“Imekua ni wiki ya huzuni sana lakini imetupatia muda wa kutafakari kuhusu kumbukumbu nzuri na hadithi za kibinafsi na tulizoshirikishana ,” Bw Tindall alisema.

Mke wa Tindall aijifungua mtoto wake wa tatu wiki tatu tu zilizopita na akamuita Lucas Philip, ambapo jina lake la kati kati alipewa kwa heshima ya Mtawala wa Edinburgh, baba yake Bw Tindall.

Katika wiki tangu alipofariki Mwanamfalme Philip akiwa na umri wa miaka 99, wanafamilia kadhaa wa familia ya ufalme wamekuwa wakichapisha picha ambazo awali hazikuwahi kuonekana.

Undated handout image released on 14/04/21 of Queen Elizabeth II and the Duke of Edinburgh with their great grandchildren. Pictured (left to right) Prince George, Prince Louis being held by Queen Elizabeth II, Savannah Phillips (standing at rear), Princess Charlotte, the Duke of Edinburgh, Isla Phillips holding Lena Tindall, and Mia Tindall.

Chanzo cha picha, Duchess of Cambridge

Maelezo ya picha,

Picha ya mwaka 2018 imetolewa na Fmilia ya Ufalme inamuonesha Malkia na Mwanamfalme Prince Philip na vitukuu saba kati ya vitukuu vyao. Vitukuu hao ni : (kuanzia kushoto kuelekea kulia )Mwanamfalme George, Mwanamfalme Louis, Savannah Phillips (akiwa amesimama), Bintimfalme Charlotte, Isla Phillips akiwa amembeba Lena Tindall, na mwisho ni Mia Tindall.

The Queen and Duke of Edinburgh seen with the Duke and Duchess of Cambridge, Prince George and Princess Charlotte at Balmoral in 2015

Chanzo cha picha, Kensington Palace

Maelezo ya picha,

Picha ya kasri la Kensington inamuonyesha Malkia na mumewe Mtawala wa Edinburgh wakiwa pamoja na Mtawala wa Cambridge na Mkewe, Mwanamfalme George na Bingtimfalme Charlotte katika Balmoral mwaka 2015

The Duke of Edinburgh seen beside the Prince of Wales playing polo in 1966

Chanzo cha picha, Clarence House

Maelezo ya picha,

Mtawala wa Edinburgh anaonekana kando ya Mwanamfalme wa Wales wakicheza polo mwaka 1966 katika picha iliyotolewa na Clarence House

Image released by Clarence House 14/04/2021 of the Duke of Edinburgh, Prince Charles and Camilla in 2011

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Clarence House pia ilitoa picha ya Mtawala wa Edinburgh akicheka na Bintimfalme wa Wales katika siku ya harusi ya Mwanamfalme William mwaka 2011

Princess Beatrice, Princess Eugenie and Prince Philip, Duke of Edinburgh at the Derby Festival in 2012

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kasri ya Buckingham ilitoa picha ya Philip akiwa pamoja na Bintimfalme Beatrice na Bintimfalme Princess Eugenie katika tamasha la Derby mwaka 2012

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *