img

Mwambusi mutaiona Yanga mpya leo

April 17, 2021

Kaimu kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema wanayanga wategemee kuiona Yanga yenye mabadiliko kuelekea kwenye mcehzo wake wa VPL wa leo Aprili 17, 2021 dhidi ya Biashara United utakaochezwa saa 1:00 usiku kwenye dimba la Mkapa.

Mwambusi amesema “Hii mechi yetu itakuwa na mabadiliko kwasababu tumeshaona nini ambacho tulikuwa tunafeli na kwanini tulikuwa hatu tumii nafasi tulizokuwa tunazipata, tumelifanyia kazi na wachezaji wameelewa na vile vile wapo tayari kucheza”.

“Mpira wetu hautokuwa wakurudi nyuma, utakuwa mpira wa direct football wakushambulia mpaka dakika za mwisho, tumejiandaa na tupo tayari kwa mapambanio”.

Mwambusi ameshangaa wanaoiondoa klabu hiyo kwenye mbiop za ubingwa na kusema “Tuna michezo 10, ligi bado haijaisha chochote kinaweza kutokea hakuna kukata tamaa”.

Yanga inategemea kuwa kosakiungo wake, Mapinduzi Balama anayeendelea na mazoez mepesi ili kuiweka sawa ilhali mlinzi wake wa kushoto, Yassin Mustapha anasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.

Kwa upande wa timu mgeni, kocha msaidizi wa klabu ya Biashara United, Marwa Chamberi amesema:

“Hatukapata matokeo kwenye michezo yetu miwili iliyopita ya nyumbani tumeambulia pointi moja, tumekuja kumbana na Yanga ambayo ni timu kubwa ila hatuiogopi au kuihofia. Tumejiandaa vilivyo kuikabili na tunategemea kupata matokeo mazuri”.

Kwenye michezo mitano ya Ligi kuu waliyokutana wawili hao tokea Biashara United ipande daraja misimu miwili iliyopita, Yanga anaongoza kwa kuwafunga maafande hao wa mpakani kwa kuwafunga mara tatu, sare moja ilhali Biashara ikipata ushindi kwenye mchezo mmoja.

Yanga ndiye kinara wa VPL wakiwa na alama 51, michezo 24 ilhali Biashara United Mara nafasi ya nne alama 40 baada ya michezo 25 Huku Yanga wakihaha kusaka ushindi baada ya kupata ushindi mmoja kwenye michezo yake saba ya mwisho, sare tano na kufungwa mchezo mmoja.

Na mchezo huu utatangazwa moja kwa moja kupitia East Africa redio kuanzia uchambuzi kabla ya mchezo saa 12:30 jioni na mchezo huo utakapoanza saa 1:00 usiku. East Africa redio inapatikana kwa masafa ya 88.1 jijini Dar es Salaam na kupitia eastafricaradio.com popote ulipo kupitia mtandao.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *