img

Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda atiwa nguvuni Rwanda baada ya kurejeshwa kutoka Marekani

April 17, 2021

  • Yves Bucyana
  • BBC Swahili, Kigali

Dakika 12 zilizopita

Beatrice Munyenyezi alitiwa nguvuni mara baada ya kufikishwa Rwanda na mamlaka za Marekani

Chanzo cha picha, RBA/Twitter

Maelezo ya picha,

Beatrice Munyenyezi alitiwa nguvuni mara baada ya kufikishwa Rwanda na mamlaka za Marekani

Idara ya Upelelezi wa makosa ya jinai nchini Rwanda imemkamata na kumshikilia Bi Béatrice Munyenyezi mara tu baada ya kusafirishwa hadi mjini Kigali na nchi ya Marekani Ijumaa usiku.

Mume wake Bwana Arsène Shalom Ntahobali na mama mkwe Nyiramasuhuko pia wanazuliwa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kimbari na mahakama ya Arusha Tanzania. Mamlaka nchini Rwanda zinasema Bi Munyenyezi anashtakiwa makosa ya mauaji ya kimbari yakiwemo kupanga na kutekeleza mauaji hayo,kuangamiza kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na ubakaji, makosa ambayo anatuhumiwa kufanyia katika mji wa Huye mkoa wa kusini mwa Rwanda.

Shirka la habari la taifa la Rwanda (RBA) limeshirikisha umma picha za tukio la kukamatwa kwa Bi Munyenyezi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kigali:

Munyenyezi, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani na mahakama nchini Marekani kwa kumpata na hatia ya udanganyifu wa kwamba hakuhusika katika mauaji ya kimbari na alipelekwa Rwanda mara tu baada ya kukamilisha hukumu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai Thierry Murangira amesema ” serikali ya Amerika haikupendelea kumbakiza kwenye ardhi yake, ikaona a heri kumrudisha Rwanda, huo ni ujumbe mkubwa”

Alisema ”kumrudisha Rwanda ni kwa manufaa ya sheria kwani tayari alikuwa amefunguliwa mashtaka kutokana na makosa anayotuhumiwa kufanya yenye uhusiano na mauaji ya kimbari”

Béatrice Munyenyezi alitiwa nguvuni mara baada ya kuwasili mjini kigali

Chanzo cha picha, RWANDA INVESTIGATION BUREAU

Munyenyezi, mwenye umri wa miaka 51 na watoto watatu, ambaye alikuwa anaishi Manchester huko New Hampshire, alikamatwa mnamo 2010 kwa madai ya udanganyifu.

Mume wa Munyenyezi Bwana Arsène Shalom Ntahobali na mama mkwe Pauline Nyiramasuhuko, tayari walipatikana na hatia ya mauaji ya kimbari na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama ya Arusha.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *