img

Mfumo Kuwekwa Wizarani Kufuatilia Vibali Vya Ajira

April 17, 2021

JESHI la Zimamoto na Uokoaji limebaini chanzo cha majanga ya moto katika shule za bweni miongoni mwake ikiwa ni wanafunzi kuchaji simu kwa kificho kwa kutumia nyaya za umeme zilizopita darini.

Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Joseph Mwasabeja, kuhusu matukio mbalimbali ambayo limefanya uokozi, imesema majanga mengi ya moto yanatokana na uzembe, hujuma na hitilafu za umeme.

“…tumebaini wanafunzi wanachaji simu kwa kificho kwa kutumia nyaya za umeme zilizopita darini, kutumia heater, kutumia pasi bila kuwa waangalifu, mishumaa wakati umeme ukikatika katika shule za bweni,” taarifa hiyo imeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika kipindi cha Januari hadi Machi, mwaka huu, jeshi limekabiliana na matukio ya moto 366 ambayo yamesababisha vifo vya watu 10 na majeruhi 30.

Shule zipatazo 16 zimeungua katika kipindi hicho cha miezi mitatu na kusababisha uharibifu wa miundombinu na kuteketea kwa vifaa mbalimbali.

Ili kupunguza majanga ya moto shuleni, taarifa hiyo imeeleza kuwa jeshi liliingia makubaliano na Chama cha Skauti Tanzania, kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto na maokozi kwa Skauti Tanzania Bara.

Baada ya kupewa mafunzo, watawafundisha wanafunzi wenzao na kazi hiyo imeshaanza na skauti kutoka katika mikoa kadhaa wanaendelea kupata mafunzo hayo.

Jeshi hilo limesema linaendelea na mikakati ya kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya majanga ya moto kwenye maeneo yote ya mikusanyiko ya watu ikiwamo masoko, nyumba za ibada, shule zote za bweni na kutwa na viwanja vya michezo.

Licha ya matukio ya moto, taarifa hiyo ya jeshi la zimamoto na uokoaji imesema katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu, limefanya uokozi katika maeneo mbalimbali zikiwamo ajali za barabarani, mafuriko, kwenye migodi, mashimo ya vyoo, mito, mabwawa, baharini pamoja na maeneo mengine.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *