img

Mazishi ya aliyekuwa Mume wa Malkia Elizabeth kufanyika leo

April 17, 2021

 

Mazishi ya aliyekuwa Mume wa Malkia Elizabeth II na Mtawala wa Edinburgh, Prince Philip yatafanyika Leo Aprili 17, 2021

Idadi ya waombolezaji watakaohudhuria mazishi hayo ni 30, wakiwamo ndugu watatu wa mwanamfalme Philip kutoka nchini Ujerumani.

Wageni wote watavalia barakoa na hawatakaribiana kama inavyoelekezwa katika muongozo wa kudhibiti virusi vya corona

Watoto wanne wa Mwanamfalme Philip watalisindikiza jeneza la baba yao katika shughuli ya ibada ya mazishi hii leo.

Wanamfalme Charles, Andrew, Edward dada yao Bintimfalme Anne, pamoja na wajukuu wa Malkia Wanamfalme William na Harry, watatembea pembezoni mwa gari aina ya Land Rover ambalo litaubeba mwili wa Mwanamfalme Philip kuelekea katika kanisa la Mtakatifu George katika kasri ya Windsor

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kasri ya Buckinham, ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza saa tisa alasiri, sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.

Prince Philip alifariki Dunia April 9, 2021 akiwa na Umri wa miaka 99.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *