img

Mandzukic asamehe mshahara wa mwezi mzima

April 17, 2021

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Croatia anayeichezea AC Milan Mario Mandzukic (34) amesamehe mshahara wake wa mwezi March 2021 euro 300,000 (Tsh Milioni 834.1) baada ya kutoichezea AC Milan mchezo wowote mwezi March kutokana na kuwa majeruhi.

Pesa hizo zimepelekwa katika mfuko wa Charity wa AC Milan kwa ajili ya kusaidia vijana, Rais wa AC Milan Paolo Scaroni amempongeza kwa uadilifu na ueledi wa kiwango cha juu.

Mandzukic aliyejiunga na AC Milan January 2021 kwa mkataba miezi sita akitokea Al Duhail ya Qatar, anaweza kurejea uwanjani Jumapilii hii kuitumikia AC Milan katika mchezo dhidi ya Genoa wa Ligi Kuu Italia baada ya kupona majeraha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *