img

Kiongozi wa kijeshi wa Myanmar kuhudhuria mkutano wa ASEAN

April 17, 2021

Kiongozi wa kijeshi nchini Myanmar, Min Aung Hlaing atahudhuria mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Mataifa ya Kusini/mashariki mwa Asia, (ASEAN) ambao unatarajiwa kufanyika Aprili 24 nchini Indonesia. 

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Thaland.Viongozi kadhaa ya mataifa 10 ya ASEAN, ambapo pia Myanmar ni mwanachama, wamethibitisha mahudhirio yao katika mkutano huo utakaofanyika Jakarta, akiwemo kiongozi huyo wa kijeshi wa Myanmar.

Mataifa jirani na Myanmar yamekuwa yakipigia chapuo mazungumzo ya amani kati ya pande zinazohasimiana nchini humo kwa lengo la kuyafikisha kikomo machafuko ambayo yalitokea baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Feburuari Mosi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *