img

Kikosi cha usalama cha Urusi kinamshikilia mwanadipolomasia wa Ukraine

April 17, 2021

Shirika la upelelezi la Urusi – FSB linamshikilia mwanadiplomasia wa Ukraine, Oleksandr Sosoniuk huko St Petersburg. 

Habari hizo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax, likinukuu idara hiyo ikizungumza leo.Shirika hilo limenukuu FSB ikieleza Sosoniuk alijaribu kujinyakulia nyaraka muhimu katika mfumo wa uhifadhi wa data za utekelezaji wa sheria wa Urusi.

Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza Reuters, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine haikuweza kupatikana mara moja kwa ajili ya kuthibitisha taarifa hiyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *