img

Jose Mourinho ampotezea Pogba

April 17, 2021

 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa hawezi kujali kuhusu yale ambayo anayasema kwa sasa kiungo wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba kuhusu yeye kuwa mkosoaji.

Pogba aliwahi kufundishwa na Mourinho katika kikosi cha Manchester United na walikuwa na mvutano wa mara kwa mara kabla ya kocha huyo kufutwa kazi na sasa United ipo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer.

Kiungo huyo hivi karibuni alisema kuwa Mourinho alikuwa anatoa maelekezo na kukosoa pale ambapo wanashindwa kufanya hivyo kwa wakati jambo ambalo ni tofauti na kocha wao wa sasa namna anavyofanya kwa kuwa anakwenda nao sawa.

Pia kutokana na tofauti zao Mourinho alimvua kitambaa cha unahodha Pogba jambo ambalo liliongeza mvutano wake. Baada ya sare ya Tottenham kufungana mabao 2-2 dhidi ya Everton, Mourinho amesema kuwa ni masuala yake anayofikiria.  

Mourinho alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu maneno ya Pogba kupitia Sky Sports alisema:”Ninapenda kusema kwamba sijali kuhusu ambacho amekisema, sijavutiwa nacho katika yote,”.

Pogba aliweza kunyanya taji la League Cup na Europa League katika msimu wa kwanza wa kufanya kazi na Mourinho ndani ya Manchester United.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *