img

Yanga yapania kufanya kweli

April 16, 2021

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema, Yanga wanataraji kufanya kweli na kuibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa VPL dhidi ya klabu ya Biashara United Mara utakaochezwa saa 1:00 usiku kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya kupata bao kwenye moja ya mchezo wa VPL mwaka huu.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Bumbuli amesema:

“Maandalizi yanaenda vizuri, tunashukuru Mwenye enzi Mungu. Baada ya mchezo uliopita, Mwalimu ameona mapungufu na amekuwa anafanyia kazi yale aliyoyaona na sisi kama Uongozi tuna muunga mkono kuhakikisha kwamba anayarekebisha”.

“Na tunakwenda kwenye mchezo huo tukiwa na nguvu mpya, Ari mpya ili tuweze kupata matokeo chanya ya ushindi ili turejee kwenye ari yetu y akuwania ubingwa”.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao ndiyowa mara ya mwisho wawili hao kukutana, Yanga aliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 bao lililofungwa na mshambuliaji wake Michael Sarpong kwenye dimba la Karume mkoani Mara.

Yanga ndiye kinara wa VPL kwasasa akiwa na alama 51 utofauti wa alama 4 na Azam anayeshika nafasi ya pili ilhali Maafande wa mpakani, Biashara United Mara wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama 40 baada ya kucheza michezo 25.

Michezo mingine itakayopigwa kesho, Aprili 17, 2021 ni pamoja na, Coastal Union ambao watawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Mkwakwani na Kagera Sukari watakuwa wageni wa Mtibwa Sukari saa 10:00 jioni mkoani Morogoro.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *