img

Waziri Mkuu wa Haiti Joseph Jouthe atangaza kujiuzulu

April 16, 2021

Waziri Mkuu wa Haiti Joseph Jouthe alijiuzulu kutoka wadhifa wake ambapo maandamano ya ghasia yamekuwa yakiendelea kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita.

Kulingana na ripoti ya Sputnik, wakati Jouthe hakuelezea sababu yoyote ya kuacha wadhifa wake, aliandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter uliosema,

“Nimewasilisha ombi langu la kujiuzulu kwa Rais Mheshimiwa Jovenel Moise. Ni heshima kwangu kutumika kama Waziri Mkuu wa nchi yangu.”

Jouthe, ambaye ombi lake la kujiuzulu lilikubaliwa na Moise, aliwashukuru wenzake ambao amekuwa akifanya nao kazi tangu Machi 2, 2020.

Rais Jovenel Moise, ambaye alitoa taarifa kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, alisema:

“Waziri Claude Joseph ameteuliwa kama Waziri Mkuu ili kuepusha shida ambazo zinaweza kusababisha ukosefu wa uaminifu na utulivu wa kisiasa na taasisi ya nchi yetu katika kudumisha njia za mazungumzo ya kisiasa.”

Claude Joseph alikuwa akihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje.

Maandamano yamekuwa yakifanyika nchini humo tangu Oktoba 2020, ambapo raia wanamtaka Moise aondoke madarakani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *