img

Waziri Mkuu atoa maagizo haya kwa wizara hizi

April 16, 2021

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maagizo kwa wizara na taasisi zinazohudumia wawekezaji kuhakikisha wanatoa huduma stahiki na taarifa muhimu na kuhakikisha wanaondoa usumbufu ikiwemo rushwa .

Waziri Majliwa amesema hayo leo akiwa anajiba hoja zilizojitokeza katika bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu katika majadiliano ya bungeni ambapo amesema tathimini ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwekezaji ya 1996 imeshakamilika.

“Ninatoa maelekezo kwa wizara na taasisi zote zinazowahudumia wawekezaji kuhakikisha wanawezesha uwekezaji katika maeneo yao kwa kutoa huduma stahiki na taarifa muhimu zinapatikana kwa wakati na kuondoa usumbufu ukiwa unaambatana na maombi ya rushwa na urasimu hili tutalisimamia, Nasisitiza watendaji wajiepushe na uombaji wa rushwa , urasimu usiokuwa wa lazima katika kuwahudumia wawekezaji ili kujenga imani baina ya sekta ya umma na sekta binafsi ili tuweze kuzungumza lugha moja” amesema Waziri Majaliwa

Aidha Majaliwa amewatoa wasiwasi watanzania kuwa mkakati wa uenzi wa makao makuu ya nchi Dodoma unaendelea na Dodoma itaendelea kuwa makao makuu ya nchi huku akikaribisha wawekezaji katika jiji hilo kwa ajili ya kuwekeza.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *