img

Virusi vya Corona:Kuna wanaosumbuliwa akili kwa kuwaza tu kwamba wana maradhi,na janga la Corona limefanya hali kuwa mbaya

April 16, 2021

Dakika 10 zilizopita

'Health anxiety took all logic away from me', says Cherelle Farrugia

Chanzo cha picha, CHERELLE FARRUGIA

Maelezo ya picha,

Cherelle Farrugia anasema wasi wasi wa kiafya nusura umfanye apoteze maisha yake

Watu ambao huogopa kupatwa na marajhi hupuuzwa kama walio na matatizo fulani ya kiakili . Lakini kwa wengine janga la corona limewafanya kuanza kupata hofu kuhusu afya yao na kuchukua hatua ambazo kwa kawaida zingeonekana ni za kushangaza .

Mnamo Machi mwaka wa 2020 Ben aliacha kazi yake ya dereva wa basi .

Wakati wowote alipokuwa hayupo kwenye zamu hakuacha kufikiria jinsi mmoja wa abiria wake anayeshuku alikuwa na Covid-19 na kumuambukiza. Ingawa alikuwa mchanga na mzima wa afya na uwezekano kuugua ulikuwa mdogo , alikuwa amesisitiza juu ya wazo kwamba ataambukizwa na kufa.

Ndani ya wiki mbili, Ben alikuwa amehama kutoka kwa familia yake huko Birmingham na kuingia katika nyumba ya wanafunzi ambayo marafiki zake walikuwa wameondoka. “Niliendelea kufikiria juu ya kuwa mahali ambapo hakuna mtu alikuwa akienda au kutoka,” anasema.

Licha ya kuondoka nyumbani na kuacha kazi, wasiwasi wake juu ya kuambukizwa bado ulitawala mawazo yake. “Ningeamka na kuangalia ikiwa mwili wangu ulikuwa sawa,” anasema.

” Nilikuwa nimechoka nilikuwa na hakika kabisa kuwa nilikuwa nao. Niliogopa kwenda dukani. Niliepuka tu kwenda nje na kuwaona watu. Yote ilikuwa hofu ya ‘je hiki kikitokea?’ Ben alikuwa akipata wasiwasi juu ya afya yake.

Nusura hofu hiyo ichukue maisha yangu

Ingawaje sote wakati mwingine huwa tuna wasiwasi juu ya afya zetu, au kutafuta daalili katika google , wasiwasi wa kiafya ni hali inayotambuliwa ambapo mtu anakuwa na hofu kubwa juu ya afya yake kupindukia .

Inatambulika kwa mtu ambaye wakati wote anaangalia daalili za magonjwa katika mwili wake na hata kufanya utafiti kuhusu maradhi mbali mbali ili kuepuka lolote linaloweza kumtia katika hatari ya kuambukizwa .

Hali hiyo imewakumba watua wengi mwaka huu baada ya kutokea kwa janga la Corona

Wengi wameshindwa hata kuondoka kutoka nyumba zao au hata kufungua madirisha kwa kuhofia kuambukizwa . Wengine kama Ben hata wameacha kazi .wengine wanatumia muda wao kusafisha nyumba zao kwa kemikali ili kuua bakteria na viini wanavyoshuku vinaweza kuwaletea maradhi.

” Wakati watu wanaposema ni suala dogo si kweli kwa sababu nusura lichukue maisha yangu’ anasema Cherelle Farrugia, kutoka Cardiff, ambaye anaendesha programu ya Youtube yenye kuwapa msaada watu wenye wasi wasi kuhusu afya zao .

Kwanza alijikuta na hali hiyo miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya kupata uvimbe mdogo . Mara tu ilipothibitishwa kwamba hali si mbaya alianza kujiambia ana saratani ya matiti na hata uvimbe wa ubongo na zaidi. Hakuwa na wasiwasi tu juu ya kuugua, lakini hakika alikuwa akijiona akifa na hakuna mtu aliyesikiliza.

“Mimi ni mtu mwenye busara na akili lakini wasiwasi wa kiafya uliniondolea busara yote ya kufirikia vizuri ,” anaelezea. Hofu hiyo ya kila wakati ilikuwa mbaya sana na mara kwa mara aliishia katika kituo cha masuala ya afya ya akili kwani alishindwa hata kufanya kazi.

“Nilianza kufirikia kuhusu kujiua, jambo ambalo lilikuwa la kushangaza kwa sababu nilikuwa najaribu kuepuka kifo,” anasema. “Lakini ikawa mbaya sana kwamba sikuweza kuishi mawazo tena. Hakuna nilichofanya kilichonituliza.” Na janga la Corona lilifanya mambo kuwa mabaya zaidi.

Adui usiyemuona

Wasiwasi wa kiafya kwa ujumla hushughulikia maeneo mawili – hofu kwamba tayari una magonjwa au uogope kuwa unaweza kuugua. Wakati wa janga hilo, mwisho uliathiri kila mtu. Lakini kama magonjwa mengi ya akili, ni hatua moja tu .

Wakati watu wengine hawafikirii kuhusu mambo kama hayo ya kuugua , kwa wengine ndio tu jambo wanalofikiria. Hatahivyo idadi ya wale wanaopata wasiwasi wa kiafya imeongezeka.

Dr Rob Willson, mtaalamu wa masuala ya tabia anasema “hajawahi kuwa na maswali zaidi” juu ya wasiwasi wa kiafya. Mtaalamu mwingine aliiambia BBC alikuwa ameratibiwa kuwahudumia watu kwa miezi michache ijayo .

Sijaweza kutoka nje kwa muda mrefu

Chanzo cha picha, Myra Ali

Maelezo ya picha,

Sijaweza kutoka nje kwa muda mrefu

Lakini kutafuta matibabu sio sulushisho ambalo hupunguza wasiwasi. “hakikisho kamwe huwa halileti utulivu ndivyo tunavyosema kila wakati,” anaelezea mwanasaikolojia wa kliniki Dr Marianne Trent, ambaye anaendesha mazoezi ya kibinafsi ya afya ya akili huko Coventry. “Ulimwengu wao unakuwa mdogo sana, lakini dhiki yao bado ni kubwa sana.”

Virusi vya corona haswa imeleta shida kwa wale walio na wasiwasi wa kiafya.

Dalili kama kupungua kwa pumzi inaweza kuwa dalili ya wasiwasi na Covid, na hizo mbili zinaweza kuunda mzunguko mbaya. Kadiri unavyozidi kuwa na wasiwasi ndivyo unavyopata “ushahidi” zaidi kuwa wewe ni mgonjwa.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *